WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango ametaka kuwapo na uratibu
wenye maslahi mapana katika biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China.
Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.
Alisema mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na China ambayo ni ya
kihistoria yasitumike vibaya bali yanahitaji kuratibiwa kiuangalifu kwa
maslahi ya pande zote mbili.
Aliwataka washiriki wa mkutano huo wa mwaka kujadili kwa makini namna ya
kuratibu vizuri vitega uchumi na biashara kwa manufaa ya nchi zote
mbili.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba kwa
niaba ya Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati
akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]
Alielezea kufurahishwa kuwapo na mada mbalimbali zinaozungumzia biashara
na uwekezaji kati ya Tanzania na China na kusema mada hizo zitumike
vyema kuweka misingi mizuri yenye manufaa kwa pande zote mbili.
Aidha aliipongeza ESRF kwa kuona haja ya kuwapo kwa mazungumzo ya aina
hiyo na kusema kupitia tafiti mbalimbali taifa hili litaenda mbele
katika kujenga uchumi wa viwanda.
Mkutano huo unaohusisha washiriki mbalimbali wa ngazi za juu wa biashara
na uwekezaji kati ya Tanzania na China umeitwa kama sehemu ya mchango
wa ESRF katika ujenzi wa uchumi wa viwanda wa Tanzania.
“Sisi serikalini tunaridhishwa na juhudi zinazofanywa na taasisi za
kitafiti kama hii zenye lengo la kusaidia juhudi za serikali za
kuhudumia watu wake na kuongeza ustawi” alisema Mpango.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),
Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6
wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]
Mkutano huo ambao unazungumzia mahusiano ya kibiashara na uwekezaji
umeelezwa na Mh. Dk Mpango kuwa moja ya mikutano inayotoa fursa za
kuangalia uwekezaji wenye tija unaozingatia maslahi mapana ya mataifa
husika.
Alisema Tanzania na China zina uhusiano mzuri wa kihistoria na hadi sasa
na kwamba kinachostahili ni kuoanisha uhusiano huo na kuuweka katika
hali bora zaidi za kunufaisha pande zote mbili.
Baadhi ya miradi mikubwa ambayo Tanzania imesaidiwa na China ni pamoja
na ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na kiwanda cha Urafiki;
kuanzishwa kwa shamba la mpunga la Mbarali; kiwanda cha sukari cha
Mahonda na mgodi wa mawe wa Kiwira.
Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo akizungumza machache kabla
ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]
Kwa sasa China ni moja ya taifa lililo na uwekezaji mkubwa nchini
Tanzania pia ikifanya shughuli nyingi za ujenzi zenye gharama kubwa kama
daraja la Kigamboni na barabara.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo, akimkaribisha
Mheshimiwa Waziri Mpango alisema kwamba alisema kwamba mkutano huo
umeandaliwa kwa pamoja kati ya ESRF na Chuo kikuu cha Kilimo cha China.
Alisema mkutano huo umewaleta pamoja wanazuoni wa Kichina na Kitanzania
kuangalia mahusiano yaliyopo na kutengeneza mustakabli bora wa namna ya
kushirikiana.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk. Tausi Kida amesema kwamba mkutano huo ni sehemu ya juhudi za
kusaidia serikali kwa njia ya utafiti ambapo majibu yanatumiwa
kutengeneza sera au majibu ya changamoto mbalimbali.
Mkutano huo ulifungwa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed
Salim.
Mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini Tanzania anayeshughulikia wa
Masuala ya Uchumi na Biashara, Lin Zhiyong akizungumza kwa niaba ya
balozi wa China wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf
Mkenda akiwasilisha mada inayohusu namna watanzania wanavyoweza
kunufaika na fursa za kibiashara na uwekezaji China wakati wa mkutano wa
6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania
na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka China na Tanzania
waliohudhuria mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti ya Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo China (CIDRN), Prof. Dr.
Li Xiaoyun akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa
mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki akizungumzia namna
ambavyo watanzania wanaweza wakafaidika na fursa za biashara na
uwekezaji nchini China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwasilisha mada inayohusu
mahusiano ya kibiashara ya uwekezaji kati ya Tanzania na China kwa
mtazamo wa Serikali za Mitaa wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, Balozi wa Tanzania nchini China, Mh.
Mbelwa Kairuki, Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim, Mwenyekiti
wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni za Infotech Investment, Ali Mfuruki wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zikiwasilisha wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkutano ukiendelea.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki pamoja na Waziri
Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokua zikiwasilishwa katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Profesa Humphrey Moshi kutoka idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam akiwasilisha mada inayohusu uhusiano wa China na Tanzania
katika masuala ya uwekezaji na biashara wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka
wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Maalum ya Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu
Joseph Simbakalia akichangia maoni wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa
ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanachama wa Chama cha Wanafunzi walisomea China (CAAT), Linas Kahisha
akielezea uzoefu wake katika fursa za kibiashara nchini humo katika
mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati
ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka Tanzania na Chini waliohudhuria
mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati
ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango,
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiwa katika picha
ya pamoja na wanafunzi watafiiti kutoka nchini China.
Home »
» ESRF YAANDAA MKUTANO KUJADILI BIASHARA NA UWEKAZAJI KATI YA TANZANIA NA CHINA
ESRF YAANDAA MKUTANO KUJADILI BIASHARA NA UWEKAZAJI KATI YA TANZANIA NA CHINA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment