Home » » TARURA YAPONGEZWA KWA KUFANYA VIZURI BARIADI, MWAKA WA FEDHA 2023/2024

TARURA YAPONGEZWA KWA KUFANYA VIZURI BARIADI, MWAKA WA FEDHA 2023/2024

TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi inahudumua barabara zenye urefu wa jumla ya km 607.49. Hayo yamesemwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne, kilichofanyika tarehe 30/7/2024 ndani ya ukumbi wa halmashauri, kijiji cha Isenge.

Akiwasilisha taarifa hiyo, Kaimu Meneja TARURA, Mhandisi, Khalid Mang'ola amesema kwa  km 607.49, barabara za Mkusanyo ni km 199.79, barabara za Mlisho ni km 353.23 na barabara za Jamii ni km 54.47.

" Kati ya barabara hizo km 224.77 sawa na 37% zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka, km 219.54 sawa na 36.14% ni za wastani na km 163.18 ambazo ni 26.86% ziko katika hali mbaya na zinapitika kwa shida au hazipitiki kabisa msimu wa mvua ( masika)." Mhandisi,Khalid Mang'ola.
   
Ameongeza kuwa, mpaka sasa  kwa utekelezaji wa matengenezo ya barabara kwa mwaka 2023/2024, km 45 za barabara kwa matengenezo ya kawaida zimekamilika, ujenzi wa makalvati 8, daraja dogo 1 na kalvati 14 za kipenyo cha 900mm vimekamilika kutoka Mfuko wa Barabara (RF).
Matengenezo kupitia Mfuko wa Fedha za Jimbo  yamekamilisha ujenzi wa kalvati 12 na madaraja madogo ya mawe 4.Pia km 10 zimekamilika ikiwemo km 6 za moramu.
Kupitia Mfuko wa Tozo, barabara ya km 1.38 ya Dutwa- Mwamondi ujenzi wa kiwango cha lami unaendelea na kupitia Mfuko wa Fedha za Maendeleo, ujenzi wa barabara kiwango cha lami m 750 ya Isakalyamhela-Nkololo kazi inaendelea.

Aidha ujenzi wa daraja la Mwadobana liloloko mto Sangai lenye urefu wa m 36 umeshakamilika. Ameeleza Mhandisi huyo.

Baraza  limempongeza Kaimu Meneja huyo na taasisi yote kwa ujumla kwa uwasilishaji mzuri wa taarifa na uwajibikaji ambao kihalisi umenufaisha wananchi.

Kuanzia kipindi cha Mwezi Julai, 2023 hadi Juni 30, 2024, TARURA Bariadi imepokea tsh. 402, 799, 909.00 kutoka Mfuko wa Barabara ( RF), Fedha za Jimbo na Fedha za Tozo kutoka Serikali Kuu.

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa