WAPENZI WA MUZIKI WA INJILI WAFURAHI UJIO WA TAMASHA LA PASAKA BARIADI MKOANI SIMIYU,DODOMA JUMAPILI HII.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akisalimia mashabiki akiwa na waimbaji pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Bariadi na mkoa wa Simiyu katika tamasha la Pasaka lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu
Ilikuwa ni buradani na furaha kwa wakazi wa Bariadi na vitongoji vyake wakati waimbaji wa nyimbo za injili walipokuwa wakitumbuiza uwanjani hapo
Baadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasa hilo
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akizungumza na Wakazi wa Bariadi waliojitokeza kwenye tamasha la Pasaka lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakiburudika wakati waimbaji wa nyimobo hizo walipokuwa wakitumbuisha katika tamasha hilo
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiendelea kuwateka mashabiki wake katika tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba kibao chake kipya cha “Lazima Wakae” huku akicheza na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka katika tamasha la Pasaka lililofanyika jumatatu ya Pasaka kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Kwaya ya Vijana KKKT-Kimanga wakiimba mbele ya wakazi wa mji wa Bariadi katika uwanja wa Halmashauri,siku ya jumatatu ya pasaka.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Joshua Mlelwa akiimba mbele ya mashabiki wake ndani ya uwanja wa Halmashauri mjini Baridi,ndani ya jumatatu ya Pasaka mkoani Simiyu.
Washabiki wa muziki wa Injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo
Mwimbaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu Sifaeli Mwabuka akiwaimbisha washabiki wake mapema mwishoni mwa wiki jumatatu ya pasaka ndani ya uwanja wa Halmashauri mjini Bariasi mkoani Simiyu.Tamasha hilo lilianzia mkoani Mwanza na baadaye kufanyika simiyu na jumapili hii ndani ya mkoa wa Dodoma katika uwanaja wa Jamuhuri.
Wapenzi wa muziki wa Injili wakifurahia waimbaji katika tamasha hilo la Jumatatu ya pasaka mjin Bariadi mkoani Simiyu.
Mwimbaji machachari wa nyimbo za Injili Martha Baraka akiimba pamoja na mashabiki wake
Baadhi ya Wapenzi wa nyimbo za Injili wakishangilia vilivyo mara baada ya muimbaji Martha Baraka kushuka jukwaani na kuwafuata mashabiki wake uwanjani
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba kibao chake kipya cha “Lazima Wakae” k
huku akicheza na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka katika tamasha la Pasaka lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu huku likihudhuriwa na mashabiki lukuki wa mji huo.

Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiendelea kuwateka mashabiki wake katika tamasha hilo lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.


Baadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakiburudika wakati waimbaji wakifanya vitu vyao katika tamasha hilo.


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akicheza na Mc wa tamasha hilo MC Mwakipesile na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu pamoja na wasanii wa Rose Muhando katika tamasha la Pasaka lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi katika tamasha la Pasaka lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akisalimia mashabiki akiwa na waimbaji pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Bariadi na mkoa wa Simiyu katika tamasha la Pasaka lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akiwa na viongozi wenzake pamoja na waimbaji pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Bariadi na mkoa wa Simiyu katika tamasha la Pasaka lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiy.


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion katika tamasha la Pasaka lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion wakimisikiliza MC Mwakipesile alipokuwa akimkaribisha mkuu wa mkoa huyo katika tamasha la Pasaka lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu


Mwimbaji Dan M kutoka nchini Kenya akiimba na mashabiki wake katika tamasha hilo.


Mwimbaji Jesca Honore naye akafanya jambo katika tamasha hilo.


Picha zikionyesha baadhi ya mashabiki wakifuatilia tamasha hilo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion akizungumza na watoto na vijana mbalimbali ambao walikuwa nje ya uwanja wakiwa hawana kiingilio katika tamasha hilo nambapo baadaye aliwakati tiketi na kuwagawia wakaingia kwenye tamasha.
Suifaeli Mwabuka akiimba na mashabiki wake.
Joshua Mlelwa hapo hampigi mtu teke bali anacheza na mashabiki wake kama unavyowaona.
Moja ya Kwaya kitumbuiza katika tamasha hilo.

KUELEKEA MTIHANI WA TAIFA MEI 2018 WANAFUNZI 1003 KIDATO CHA SITA SIMIYU WAPIGA KAMBI YA KITAALUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wanafunz wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Baadhi ya walimu mahiri 40 waliochaguliwa kufundisha na kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha sita (kutoka shule 11 mkoani Simiyu) na Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kambi ya  Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt.Seif Shekalaghe akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa wa Simiyu wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani humo. 
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.




Na Stella Kalinga, Simiyu

Takribani wanafunzi 1003 wa Kidato cha sita kutoka shule za Sekondri 11 zenye kidato cha tano na sita Mkoani Simiyu, wamepiga kambi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na Shule ya Sekondari Binza, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa ambao unatarajia kufanyika mapema mwezi Mei mwaka huu.

Akifungua kambi hiyo Aprili 03 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema ili mkoa huo uweze kushindana na kufanya mageuzi katika Uchumi ni lazima kuwekeza katika elimu.

“Kama wanafunzi wetu wanakaa makambi ya michezo ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa kwa nini wanafunzi hao hao wasikae kambi kwa ajili ya maendeleo ya taaluma; tukitaka kufanya mageuzi ya Mkoa huu ni lazima tuweke nguvu kwenye elimu, maeneo yenye uchumi mzuri wamewekeza sana  kwenye elimu” alisema Mtaka. Aidha, Mtaka awataka wanafunzi wote wa kidato cha sita kuwasikiliza walimu watakaokuwa wakiwafundisha na kuwaelekeza na akawataka kujiamini wakati wa mtihani wao wa mwisho.

Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema Mkoa huo una mpango wa kuondoa daraja la nne na sifuri katika matokeo ya Mitihani ya Taifa, hivyo wanayo matumaini makubwa kuwa, kupitia makambi hayo ya kitaaluma Mkoa utaweza kufikia lengo hilo kwa matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.

“ Tumeamua kuwaleta pamoja wanafunzi ili waweze kunyanyuka kama kundi moja la mama mmoja (Simiyu) na kuweza kupandisha ufaulu, tumewaleta hapa ili kuweza kunyanyua morali wa kazi kuwaleta pamoja anayeweza na asiyeweza ili tuweze kunyanyuka pamoja kama kundi” alisema Mwl.Nestory.

Amesema katika siku 10 za kambi wanafunzi wa kidato cha sita watapitishwa katika miiko ya watahiniwa wakati wa mitihani kwa kuwa mkoa wa Simiyu unapinga suala la udanganyifu kwenye mitihani, watapitishwa katika maswali na mada ambazo baada ya tathmini ilionekana hawakufanya vizuri katika mtihani wa kanda na mtihani wa Mkoa.

Akizungumza kwa niaba ya walimu mahiri 40 ambao watakuwa wakiwafundisha na kuwasaidia wanafunzi hao, Mwl.Majaliwa Chibona wa Shule ya Sekondari Mwandoya wilayani Meatu amesema, wamejipanga kuwasaidia wanafunzi katika kuwapa mbinu na mikakati mbalimbali itakayowasaidia kujiandaa na mitihani wao wa mwisho ili waweze kufaulu.

Nao baadhi ya wanafunzi wamesema kambi hiyo itawasaidia sana katika kuwajengea hali ya kujiamini kwa kuwa watasaidiwa na walimu katika maeneo yote yanayoonekana magumu kwao, watasaidiana wa kwa wao kupitia makundi na watapewa mbinu zitakazowasaidia kujiandaa vema na hatimaye kufanya vizuri.

WAZIRI KABUDI AWATAKA WASAJILI WA VYETI VYA KUZALIWA MIKOA YA SIMIYU, MARA KUZINGATIA UMAKINI NA UZALENDO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(wa tatu kushoto) akizindua Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati) akionesha nakala ya cheti cha kuzaliwa kinachotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri huo na kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimkabidhi mkazi wa Manispaa ya Musoma cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake mwenye umri wa chini ya miaka mitano, mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa mikoa ya Simiyu na Mara, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini (RITA), Bi. Emmy Hudson akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, uliofanyika Uwanja wa Shule ya msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa salama za Mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma ya Asili cha Wagoyangi kutoka Maswa mkoani Simiyu wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mikoa ya Simiyu na Mara mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma.
Na Stella Kalinga, Simiyu

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wasajili wa vyeti vya kuzaliwa kupitia mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwenye mikoa ya Simiyu na Mara, kufanya kazi hiyo kwa umakini na uzalendo mkubwa katika kuhakikisha wanawasajili watoto wenye sifa.

Waziri Kabudi ametoa rai hiyo Machi 20 wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa, katika mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

“Mikoa ya Mara na Simiyu ina muingiliano mkubwa sana na wananchi wa nchi jirani hivyo wasajili wawe makini na watangulize uzalendo wakati wa kutekeleza mpango huu, tusisajili mtoto ambaye hahusiki na pale ambapo tuna mashaka kuwa mtoto huyo anaweza kuwa wa nchi za jirani, tutoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika ili hatua za kiusalama zichukuliwe” alisema Profesa Kabudi.

Amesema kuwa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano unafanyika bila malipo hivyo wasajili wasitumie kwa namna yoyote mpango huo kama fursa ya kujipatia fedha kwa udanganyifu.Aidha, Waziri Kabudi ameahidi kutoa tuzo maalum kwa mkoa (kati ya Simiyu na Mara) utakaofikia asilimia 80 ya lengo la usajili kwa kipindi cha miezi miwili tangu usajili ulipoanza na wakati huo huo akawataka Viongozi wa Taasisi zote Umma kuvitambua vyeti vitakavyotolewa chini ya mpango huo kwa kuwa ni vyeti halali

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini (RITA) Profe. Hamis Dihenga amesema kupitia mpango wa usajili na kutoa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, RITA inakusudia kusajili jumla ya watoto 735, 545 katika mikoa ya Simiyu na Mara kwenye vituo 463 (Mara) na Vituo 324 (Simiyu).

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mhe.Annarose Nyamubi akiwasilisha taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe.Adam Malima amesema hadi sasa Mkoa huo umesajili jumla ya watoto 78, 625 na watahakikisha watoto wote wanaopaswa kusajiliwa wanasajiliwa ndani ya miezi miwili na baadaye kuendelea na usajili kwa watoto watakaozaliwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga, akitoa salamu za Mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amesisitiza wananchi kutambua umuhimu wa kuwasajili watoto wao ili waweze kutambulika, kupewa vyeti vya kuzaliwa na Serikali iweze kupata takwimu sahihi.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Watoto (UNICEF) hapa nchini ambao ni miongoni mwa wafadhili wa mpango huu, Bi. Maud Droogleever , amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano wanasajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.

Baadhi ya wananchi wa Mikoa ya Simiyu na Mara walioshirikia katika Uzinduzi wa Mpango huo wameishukuru Serikali kwa kuleta mpango huo kwa kuwa umewarahisishia huduma ya kupata vyeti vya kuzaliwa kwa kuwasogezea huduma hiyo katika Ofisi za kata tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wanalazimika kufuata huduma hiyo katika Ofisi za Wakuu wa Wilaya
 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa