Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli ambao
utafaidisha vijiji vitatu, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt.
Raphael Chegeni.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwasalimia wananchi wa Masanza Kona, Kiloleli wilaya ya Busega mkoani
Simiyu.
Mbunge
wa Jimbo la Busega Dkt. Raphaele Chegeni akizungumza mbele ya Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kusalimia wananchi
waliojitokeza kwa wingi barabarani eneo la Nyashimo kumsalimia Makamu wa
Rais ambaye ameanza ziara ya siku tano mkoani Simiyu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za Viongozi wa Mkoa katika
eneo la Nyaumata, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewataka Viongozi wa mkoa wa Simiyu kuhakikisha kila shule ya sekondari
inayojengwa inajengwa ikiwa na maabara.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi Lamadi wilaya ya
Busega mkoani Simiyu ikiwa siku yake ya kwanza ya ziara ya siku tano
mkoani humo.
Makamu
wa Rais ambaye alianza ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi
wa mradi wa maji uliopo Kiloleli ambapo mradi huo ukikamilika utasaidia
kupatikana kwa maji safi na salama kwa vijiji vitatu na utagharimu
shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambapo ujenzi wake umefikia asilimia
80%.
Makamu
wa Rais aliwapongeza wananchi kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya
awamu ya tano katika uwekezaji na uendelezaji wa viwa nda ambapo mpaka
sasa kuna viwanda 14 vya usindikaji wa pamba na viwanda vidogo vidogo
vya usindikaji mazao 1,035.
“Nawapongeza kwa mkakati wa kuzalisha bidhaa za afya zinazotokana na pamba na maji ya drip”
Makamu
wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa hadi mwisho wa mwezi huu chupa
milioni 2 za dawa za kuuwa wadudu wanaoshambulia pamba zitakuwa
zimesambazwa.
Mwisho Makamu wa Rais aliwataka Viongozi na Watendaji kushirikiana na wananchi kwani ushirikiano
Katiak Ziara hiyo Makamu wa Rais aliweka pia jiwe la msingi la ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Serikali zilizopo Nyaumata.
0 comments:
Post a Comment