
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akisalimiana na Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini
Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi Mkoani Simiyu.

Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akifuaahia jambo na Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kumaliza
mahojiano na waandishi wa habari wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.

Wajumbe
wa Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa
Simiyu za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,
IGP Simon Sirro(hayupo pichani) katika kikao alichofanya akiwa ziarani
mkoani humo.

Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro akisalimiana na Katibu
Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Chele Ndaki mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi
kwa ajili ya ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu

Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro (kulia) na Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa huo wakati wa ziara yake mkoani humo.

Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro (kulia) akizungumza na
Kamati ya Ulizi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani
humo,(baadhi ya wajumbe hawapo pichani).

Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro akisalimiana na Katibu
Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Chele Ndaki mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi
kwa ajili ya ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu

Kaimu
Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu(kulia) akisalimiana na Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini
Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu

Katibu
Tawala Msaidizi Sehemu ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Simon Maganga(kulia) akisalimiana na Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini
Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu.
……………………………………………………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini Inspekta Generali Simon Sirro amesema
Makamanda wa Polisi wa Mikoa wataendelea kubaki katika vituo vyao vya
kazi endapo watatimiza wajibu wao na kupunguza uhalifu katika mikoa yao.
IGP
Sirro ameyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu katika
mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kamaliza mazungumzo yake
na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa yaliyofanyika katika Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
IGP
Sirro amesema Makamanda wa Polisi Mikoa wanapaswa kutimiza wajibu wao
katika kujali na kusimamia suala la Ulinzi na Usalama katika mikoa yao
ili wananchi wakae kwa amani na mali zao ziwe salama.
“
Moja ya lengo la ziara yangu ni kuwakumbusha askari wa jeshi la polisi
uwajibikaji na kuwajibika ni pamoja na kulinda watu na mali zao,
makamanda wa polisi mikoa nimewaambia kamanda ataendelea kukaa kwenye
mkoa ule kama uhalifu utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa” amesema Sirro
Inspekta
Sirro amesema ziara yake pia imelenga kuwakumbusha askari majukumu yao
katika kuhakikisha wanawajibika kutimiza kiapo chao na kutenda haki ili
wananchi waendelee kuliamini Jeshi la Polisi.
Kiongozi
huyo pia ameelekeza viongozi wa jeshi la polisi wasiwanyime haki ya
dhamana watu wenye makosa ya kawaida ambayo yana dhamana isipokuwa kwa
makosa makubwa yakiwepo ya mauaji, kughushi na mengine yanayohitaji
upelelezi.
Kuhusu
suala la kuwepo kwa mahusiano mabaya kati ya baadhi ya Makamanda wa
Polisi wa Mikoa na Waandishi wa habari, Inspekta Sirro amefafanua kuwa
Makamanda wa Polisi wa Mikoa watimize wajibu wao kama watumishi wa Umma
kwa kuwajali waandishi kama wanavyowajali wateja wengine kwa kufuata
sheria na akawataka waandishi wa habari wafuate sheria, kanuni na
taratibu pasipo kuvuka mipaka.
Akakimkaribisha
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini, katika Mkoa wa Simiyu Mkuu wa Mkoa
huo, Mhe.Anthony Mtaka amemshukuru Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo,
Boniventure Mshongi na Jeshi la Polisi kwa ujumla kwa namna
wanavyoshirikiana katika suala la ulinzi na usalama.
Aidha,
amemuomba Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini kuona uwezekano wa
kusaidia kujenga majengo ya Ofisi na nyumba za makazi kwa ajili ya
Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.
Inspekta
Simon Sirro amewasili Mkoani Simiyu akitokea Mkoani Mara akiwa katika
ziara yake ya kikazi ambapo pamoja na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Wilaya ambao pni Wenyeviti wa Kamati
za Ulinzi na Usalama za wilaya, pia amezungumza na viongozi na askari
wa Jeshi la Polisi mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment