Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(wa tatu kushoto)
akizindua Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa miaka mitano na
kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa
Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati) akionesha
nakala ya cheti cha kuzaliwa kinachotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi
na Udhamini (RITA) kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakati
wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri huo na kutoa vyeti
vya kuzaliwa, kwa mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika Manispaa ya
Musoma mkoani Mara.
Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimkabidhi mkazi wa
Manispaa ya Musoma cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake mwenye umri wa
chini ya miaka mitano, mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa
watoto wenye umri wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa mikoa
ya Simiyu na Mara, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo
Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini
(RITA), Bi. Emmy Hudson akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa
Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa
vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, uliofanyika Uwanja wa
Shule ya msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa salama za Mkoa wa Simiyu kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, wakati wa uzinduzi wa
Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa
vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule
ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Wasanii
wa Kikundi cha Ngoma ya Asili cha Wagoyangi kutoka Maswa mkoani Simiyu
wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye
umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya
Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya
Musoma mkoani Mara.
Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati kwa
walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mikoa ya Simiyu
na Mara mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri
chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa hiyo
uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wasajili wa
vyeti vya kuzaliwa kupitia mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa
kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwenye mikoa ya Simiyu
na Mara, kufanya kazi hiyo kwa umakini na uzalendo mkubwa katika
kuhakikisha wanawasajili watoto wenye sifa.
Waziri
Kabudi ametoa rai hiyo Machi 20 wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili
wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na kutoa vyeti vya
kuzaliwa, katika mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika Uwanja wa Shule ya
Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
“Mikoa ya
Mara na Simiyu ina muingiliano mkubwa sana na wananchi wa nchi jirani
hivyo wasajili wawe makini na watangulize uzalendo wakati wa kutekeleza
mpango huu, tusisajili mtoto ambaye hahusiki na pale ambapo tuna mashaka
kuwa mtoto huyo anaweza kuwa wa nchi za jirani, tutoe taarifa kwa
vyombo vinavyohusika ili hatua za kiusalama zichukuliwe” alisema Profesa
Kabudi.
Amesema
kuwa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini
ya miaka mitano unafanyika bila malipo hivyo wasajili wasitumie kwa
namna yoyote mpango huo kama fursa ya kujipatia fedha kwa
udanganyifu.Aidha, Waziri Kabudi ameahidi kutoa tuzo maalum kwa mkoa
(kati ya Simiyu na Mara) utakaofikia asilimia 80 ya lengo la usajili kwa
kipindi cha miezi miwili tangu usajili ulipoanza na wakati huo huo
akawataka Viongozi wa Taasisi zote Umma kuvitambua vyeti vitakavyotolewa
chini ya mpango huo kwa kuwa ni vyeti halali
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini (RITA)
Profe. Hamis Dihenga amesema kupitia mpango wa usajili na kutoa vyeti
kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, RITA inakusudia kusajili
jumla ya watoto 735, 545 katika mikoa ya Simiyu na Mara kwenye vituo
463 (Mara) na Vituo 324 (Simiyu).
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mhe.Annarose Nyamubi akiwasilisha
taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe.Adam Malima
amesema hadi sasa Mkoa huo umesajili jumla ya watoto 78, 625 na
watahakikisha watoto wote wanaopaswa kusajiliwa wanasajiliwa ndani ya
miezi miwili na baadaye kuendelea na usajili kwa watoto watakaozaliwa.
Naye Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga, akitoa salamu za Mkoa wa
Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amesisitiza
wananchi kutambua umuhimu wa kuwasajili watoto wao ili waweze
kutambulika, kupewa vyeti vya kuzaliwa na Serikali iweze kupata takwimu
sahihi.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Watoto (UNICEF) hapa
nchini ambao ni miongoni mwa wafadhili wa mpango huu, Bi. Maud
Droogleever , amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali
kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano wanasajiliwa
na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Baadhi ya
wananchi wa Mikoa ya Simiyu na Mara walioshirikia katika Uzinduzi wa
Mpango huo wameishukuru Serikali kwa kuleta mpango huo kwa kuwa
umewarahisishia huduma ya kupata vyeti vya kuzaliwa kwa kuwasogezea
huduma hiyo katika Ofisi za kata tofauti na ilivyokuwa awali ambapo
walikuwa wanalazimika kufuata huduma hiyo katika Ofisi za Wakuu wa
Wilaya
0 comments:
Post a Comment