Mbunge wa Jimbo la Busega, Mkoani Simiyu, Dk Raphael Chegeni ambaye kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wa ndani na nje ya nchi amefanikiwa kujenga bweni moja la wasichana katika Sekondari ya Ngasamo ikiwa ni jitihada za kuwanusuru watoto wa kike na ukatishaji masomo unaotokana na mimba pamoja na vishawishi bvingine mbalimbali.
Vitanda katika moja ya vyumba vya bweni hilo.
MBUNGE wa Busega Dr. Raphael Chegeni amefanikisha ujenzi wa bweni la
wasichana katika shule ya sekondari Ngasamo.
Bweni hilo lenye uwezo wa kuhudumu wanafunzi wa kike 48 litasaidia wasichana
kupata muda wa kujisomea na kujiepusha na adha ya kutembea mwendo mrefu wa kuja
na kurudi shuleni.
Kitendo hicho imekuwa kikwazo kwa
baadhi kuangukia mtego wa kukatisha masomo katokana na bodaboda Au lift
kuwasababishia mimba na hivyo kukatisha masomo yao.
Mbunge huyo ameweka mpango kujenga mabweni kwa shule zilizo katika mazingira
hatarishi zikiwemo Malili, Mkula, Kabita na Sogesca.
Aidha amewashukru wadau wakiwemo ubalozi wa Ireland, Canada, Tanapa na
Serikali kwa kuchangia jitihada hiz0.
0 comments:
Post a Comment