Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wadau wa Ushirika wa
Mkoa huo(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la
Mkoa huo Mjini Bariadi, (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe.Festo Kiswaga
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Kaimu
Naibu Mrajis kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Ndg.Collins Nyakunga
wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la mkoa wa Simiyu, Mjini
Bariadi
Baadhi
ya Wadau wa Ushirika Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mada mbalimbali
zilizowasilishwa mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa
huo Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Wadau wa Ushirika Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mada mbalimbali
zilizowasilishwa mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa
huo Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wadau wa Ushirika
wa mkoa huo (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la
Mkoa huo Mjini Bariadi.
Afisa
Ushirika Mkuu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Sehemu ya
Uhamasishaji na utaratibu, Veneranda Mgoba akiwasilisha mada ya
Usimamizi na Udhibiti kwa wadau wa Ushirika wa Mkoa huo(hawapo pichani)
wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa huo Mjini Bariadi.
Mwanasheria
kutoka Tume ya Maendeleo ya ushirika Kitengo cha Sheria, Donald
Deogratius akiwasilisha mada ya Sheria ya Ushirika kwa wadau wa
Ushirika wa Mkoa huo(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la
Ushirika la Mkoa huo Mjini Bariadi.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa huo unahitaji
ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi
wa kati.
Mtaka
amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa
Simiyu uliofanyika katika Ukumbi wa kanisa Katoliki Mjini Bariadi, tukio
ambalo limeshirikisha viongozi Serikali na watalaam mbalimbali ngazi ya
Mkoa na Wilaya, viongozi wa vyama vya ushirika, Tume ya maendeleo ya
Ushirika na wadau mbalimbali wa ushirika.
”
Sisi kama mkoa tuko tayari kwa yale ambayo ninyi wenzetu wa Tume ya
Ushirika mnadhani kupitia hayo tutakuwa na ushirika imara na
utakaoendeshwa kisasa, tuko tayari hata kwa kuwatoa watu wetu kujifunza
katika vyama vya ushirika vilivyofanikiwa;ushirika wa Tanzania ukiamua
Uchumi wa kati inawezekana”
Aidha,
Mtaka amesema wananchi wakielimishwa na kukubali kuungana katika vyama
ushirika wanaweza kuondokana na Umaskini, hivyo amesisitiza uwepo wa
ushirika imara wenye matokeo chanya katika maeneo muhimu ya uzalishaji,
ili hata mikoa mingine ijifunze Simiyu
“Mwalimu
Nyerere amewahi kusema namna pekee ya watu maskini kujikomboa ni
kuungana, niwasihi wanaushirika kuunganisha nguvu katika ushirika,
matajiri wanaungana kuunda makampuni yanayoweza kukopa, yakashtaki na
kushtakiwa ninyi unganeni kwenye vyama vya ushirika kujenga uchumi ”
amesema Mtaka.
Aidha,
Mtaka amesema Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) imekubali kufanya
kazi na Mkoa wa Simiyu kwa kuviwezesha vyama vya ushirika na vikundi
vilivyosajiliwa kisheria kwa kuwajengea uwezo wanachama na kuwapa mikopo
kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali, hivyo vyama vya ushirika
vinapaswa kuchangamkia fursa hiyo.
Akizungumzia
mchango wa ushirika katika utekelezaji wa Kauli Mbiu ya Mkoa”Wilaya
Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” Mkuu huyo wa Mkoa amesema vyama vya
ushirika ndivyo vyenye wazalishaji wa malighafi ya viwanda, hivyo jukwaa
la ushirika litumiwe vizuri katika kuweka mikakati ya kuimarisha vyama
vya ushirika na Viongozi wa Serikali wako tayari kuonesha ushirikiano.
Katika
hatua nyingine Mtaka amesema mkoa unaandaa andiko linalolenga
kuwakusanya wakulima na wanaushirika wote pamoja, ambapo watatumia
vyumba vya madarasa katika Shule za Serikali wanafunzi watakapokuwa
likizo kupewa mafunzo ya ushirika na kilimo na Wataalam wa Halmashauri,
Mkoa na Chuo Kikuu cha Ushirika, ili kuimarisha ushirika na kuongeza
tija katika kilimo na mifugo.
Sanjali
na hilo Mtaka amesisitiza kuwa mkoa wa Simiyu ndio unaoongoza kwa
kulima pamba hapa nchini, hivyo ni vema kukawa na ushirika wenye kuleta
majawabu kwa changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba kuondoa kero
kwa wakulima na kuongeza ubora katika uzalishaji.
Kwa
Upande wake Kaimu Naibu Mrajis kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika,
Ndg.Collins Nyakunga amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa kuonesha
nia ya kuimarisha ushirika katika mkoa huo na kuona kuwa kupitia
ushirika wananchi wanyonge wanaweza kutatua matatizo yao ya kiuchumi na
Kijamii.
Nyakunga
amesema Tume ya Maendeleo ya Ushirika itaandaa namna ambayo itautoa
ushirika katika uendeshaji wa kizamani uendeshwe kisasa, tafiti
zitafanyika kupitia Chuo Kikuu cha Ushirika kuona namna ya kuongeza bei,
thamani ya zao la pamba na ushirika mkoani Simiyu kuimarika.
Naye
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Simiyu, Ndg Mathias
Shineneko amesema Mkoa huo umejiwekea mkakati wa kuakikisha vyama vya
ushirika vinajielekeza katika kuweka taratibu za kuongeza na kuimarisha
mitaji, hisa na akiba ili kujiimarisha kiuchumi.
Wakati
huo huo Ezekiel Ganji kutoka Chama cha Msingi Sola wilayani Maswa
ameiomba Serikali kuwashirikisha wakulima wa pamba katika maamuzi ya
kupanga bei badala ya kupangwa na makampuni yanayonunua pamba na
kusisitiza kuwa katika ukaguzi wa vyama vya ushirika Serikali iangalie
uwezo wa vyama hivyo na kupunguza tozo za ukaguzi kwa kuwa vyama vingi
havina uwezo mzuri kifedha.
0 comments:
Post a Comment