Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali inaandaa mtaala wa kuongeza ustadi na ujuzi kwa watanzania wanaofanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati.
Hayo
yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya
Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Abdallah Kilima alipokuwa akikanusha habari
iliyotolewa na Gazeti la Tanzania Mpya la Oktoba 04,Mwaka huu,Toleo
namba 23 katika Ukurasa wa 4, lililokuwa na habari iliyosema “Watanzania
wateswa nchini Oman na wengine hunyofolewa figo zao na kupewa ndugu wa
waajiri wenye mahitaji”.
Kutokana
na hayo Balozi Kilima alifafanua kuwa habari hiyo haina ukweli
wowote,isipokuwa ni maoni binafsi ya mwandishi wa gazeti hilo na
hayawakilishi msimamo wa Serikali kuhusu masula ya wafanyakazi za ndani
wakitanzania nchini Omani.
Aidha,
Balozi huyo amesisitiza kuwa nia ya Serikali ya kuanzisha mtaala huo ni
katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba nazo watanzania
wanaofanyakazi za ndani nchini Oman.
“Serikali
imeazimia kutumia Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ili kutoa mtaala
utakaosaidia kutoa mafunzo kwa maana ya utaratibu na utamaduni wa nchi
wanazokwenda kufanyakazi, ili kusaidia watanzania kuwa na uelewa wa
kutosha kuhusu kazi husika na changamoto zake kabla ya kukubali
kufanyakazi hizo,” alisema Balozi Kilima
Sambamba
na hilo Serikali imeendelea kuwataka watanzania kufuata utaratibu kabla
ya kwenda kufanyakazi katika nchi hizo kwa kutumia mawakala rasmi wa
ajira walioandikishwa na mamlaka husika pamoja na kuwepo mkataba wa
ajira unaotambuliwa na Mamlaka za nchi wanazookwenda ili kuepuka
usumbufu na changamoto wanazoweza kuzipata ikiwemo kufanyiwa vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia na ukatili.
Balozi
Mwilima ameongoza kuwa katika kupata suluhisho la kudumu katika
kuwasaidia watanzania kupata fursa za ajira nje ya nchi,Wizara kwa
kushiririkiana na wadau imeendelea kufanya jitihada za kusaini
Mikataba ya Ushirikiano katika Sekta ya ajira na kazi baina ya Serikali
ya Tanzania na nchi mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment