Home » » WALIOJENGA HIFADHI YA BARABARA WABOMOLEWA.

WALIOJENGA HIFADHI YA BARABARA WABOMOLEWA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

NYUMBA zilizojengwa kandokando ya hifadhi ya barabara wilayani Bariadi mkoani Simiyu zimeanza kubomolewa jana chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi
Baadhi ya waathirika wa nyumba hizo, Frank Jilala na 
Hussein Mosha wakizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio huku wakilia kubomolewa nyumba zao, walidai hawakupewa muda wa kutosha kujiandaa kuondoa mali zao.
Mbuke Kishiwa na Ribelata Mhagama walisema kabla ya ujenzi wa barabara kubwa ya Bariadi-Lamadi kwa kiwango cha lami, walidai walifanyiwa tathimini mwaka 2012, na walikuwa wakiishi hapo tangu mwaka 1965 huku serikali ikiwaahidi pia kuwalipa fidia.

“Nilifanyiwa tathimini hapa mwaka 2012. Tangu mwaka 1965 nipo hapa eneo hili na nimekulia hapa awali barabara ilitakiwa kupita eneo la Malambo, lakini ikabadilishwa ikatakiwa kupita hapa na serikali ilinipigia hesabu ikafikia mimi nilipwe kiasi cha Sh milioni 60 kama fidia,” alisema Ribelata Mhagama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Bariadi ambapo nyumba nyingi zimeathirika, Othman Hamis alisema baadhi ya wananchi walipewa muda wa kubomoa wenyewe, lakini walikaidi licha ya kuambiwa mara kwa mara.
“Tangu majira ya asubuhi zoezi linaenda vizuri hawa wanaolia pamoja na kulalamika ni wale ambao walikaidi agizo la kubomoa wao wenyewe…wao walifikiri kuna utani kama ilivyozoeleka hapa hakuna utani ni utekelezaji tu,” alisema Hamis.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa, Albert Kent akizungumzia kazi hiyo, alisema awali wakazi hao walipewa notisi ya kuhama eneo la barabara mwaka 2012, lakini walikimbilia Mahakama Kuu iliyokuwa mkoani Tabora kupinga notisi hiyo. Alieleza kuwa kesi ilisikilizwa na kumalizika kwa serikali kushinda, hali iliyoifanya kutoa notisi nyingine mwaka 2013, ambayo nayo walikwenda mahakamani kuipinga na serikali kushinda tena.
CHANZO : GAZETI LA HABARI LEO.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa