Home » » SIMIYU WAPIGA MARUFUKU KUWA NA RIFLE.

SIMIYU WAPIGA MARUFUKU KUWA NA RIFLE.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KAMATI ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu imepiga marufuku utoaji vibali vya umiliki wa bunduki aina ya rifle mkoani hapo hasa kwa wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi ya Serengeti kutokana na kubainika kuwa silaha hizo kutumika kuua wanyama katika hifadhi hiyo.
Hata wale wote ambao walishapewa vibali vya kumiliki bunduki za aina hiyo watafanyiwa ukaguzi mkali hasa wanaoishi karibu na hifadhi mbalimbali.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Elaston Mbwilo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya uamuzi huo baada ya tukio lililotokea hivi karibuni la kutunguliwa kwa helikopta katika Pori la Akiba Maswa na watu wadhaniwa kuwa majangili.
Mbwilo alisema tukio hilo lililosababisha kifo cha rubani wake, Kapteni Rodgers Gower (37) raia wa Uingereza, imebainika kuwa bunduki hizo ndizo zenye uwezo wa kusababisha vifo kwa wanyama pamoja na binadamu kwa haraka kwa mtu ambaye atakayetumia kwa uadui.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa