Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais, John Magufuli.
Watu sita wanaodaiwa kuwa majangili, wanashikiliwa
na polisi kwa tuhuma za kuitungua helikopta ya doria na kusababisha kifo
cha rubani wake katika pori la akiba la Maswa.
Kukamatwa kwa watu hao kumekuja siku moja baada ya Rais, John
Magufuli, kutoa agizo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwakamatwa
waliohusika na tukio hilo na kufikishwa katika mkono ya sheria.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, akizungumza
na Nipashe jana alisema Rais Magufuli mbali na kusikitishwa na tukio
hilo, pia aliuakikisha umma kuwa serikali itahakikisha inaendeleza
mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zote na kuwataka wananchi na wadau
mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori kutokatishwa tama.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushy, jana alithibitisha kwa njia ya simu kukamatwa kwa watu hao.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi na wanalisaidia jeshi hilo katika uchunguzi wake kufuatia tukio hilo.
Ijumaa iliyopita, watu wasiojulikana, waliitungua helikopta hiyo
wakati ikifanya doria katika pori hilo baada ya kuwapo taarifa kwamba
majangili walikuwa wameua tembo mmoja.
Katika tukio hilo, rubani wa helikopta hiyo raia wa Uingereza,
Rodgers Gower (37) alikufa, huku mwenzake Nicky Bester wa Afrika Kusini
akinusurika.
CHANZO:
NIPASHE.
0 comments:
Post a Comment