Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BARAZA la Mamlaka ya Mji Mdogo Maswa mkoa wa Simiyu, litaanza
kukusanya kodi ya majengo ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuongeza mapato
katika mamlaka hiyo.
Uamuzi huo umepitishwa jana na wajumbe wa baraza hilo wakati wa
kujadili bajeti ya mamlaka hiyo ya mwaka 2016/2017 katika kikao
kilichofanyika mjini Maswa.
Mwenyekiti wa mamlaka hiyo, Tungaraza Lomole, alisema kuwa lengo
kubwa la kukusanya kodi za majengo ni kufanikisha maendeleo katika mji
wa Maswa, kufikia matamanio ya kuwa Halmashauri ya Mji.
Alisema huu si utaratibu mgeni kwani kodi hizi zimekuwa zikilipwa
maeneo ya mamlaka mbalimbali za miji hapa nchini na zimekuwa zikitumika
katika shughuli za maendeleo kama vile kuwapatia wananchi huduma
mbalimbali katika sekta ya elimu, afya, kilimo, mifugo na miundombinu ya
barabara.
“Kulipa kodi ni lazima kwa maendeleo ya nchi na fedha zote
zinazotumiwa na serikali katika kuwahudumia wananchi zinatokana na kodi
mbalimbali zinazolipwa na kodi hii ya majengo hutozwa chini ya Sheria ya
mamlaka za miji”, alisema.
Alisema kuwa sasa ni wakati kwa viongozi wa mamlaka hiyo hasa wale
wawakilishi wa wananchi kwenda katika maeneo yao na kuwaelimisha
wananchi juu yaulipaji wa kodi hii.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment