Home » » AKAMATWA NA BANGI KETE 300.

AKAMATWA NA BANGI KETE 300.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
POLISI mkoani Simiyu inamshikilia mkazi wa Kijiji cha Itilima ‘B’ Kata ya Kiloleli Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Siwema Paul (25) kwa kukutwa na kete 300 za bangi.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Audax Majaliwa alisema mwanamke huyo alikutwa na kete hizo nyumbani kwake akiwa amezificha. Majaliwa alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Januari 23, mwaka huu saa 9.30 alasiri wakati wa operesheni iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi hilo katika wilaya ya Busega.
Katika hatua nyingine, jeshi hilo linawashikilia watu tisa kwa kosa la kukutwa na lita 70 za pombe haramu ya gongo na mitambo ya kutengenezea pombe hiyo.
Alitaja waliokamatwa ni Monica Sekela (41) mkulima mkazi wa Busega, James Budeba (65) mkazi wa Chamgasa, Mihayo Budeba (36) mkazi wa Kalemela, Madama Bite (62) mkazi wa Meatu na Marugu Magembe (38) mkazi wa Bariadi.
Wengine ni Maduhu Wilson (38) mkazi wa Bunda mkoani Mara, Juma Magoma (34) mkazi wa Bariadi na Bela Omondi (38) mkazi wa Chamgasa, ambaye anadiwa kukutwa na mtambo wa kutengenezea pombe hiyo.
Aidha, Kaimu Kamanda huyo alisema katika operesheni inayoendelea ya ukaguzi wa pikipiki, pikipiki 36 zimebainika kukosa vielelezo halali vya wamiliki wake. Aliwataka watu walioibiwa pikipiki kufika na vielelezo halali makao makuu ya jeshi hilo mjini Bariadi kutambua pikipiki hizo.
Alisema jeshi hilo limekamata nyavu haramu aina ya kokoro za kuvulia samaki katika Kata ya Kalemela Wilaya ya Busega na linawashikilia watu wawili, Leticia Shadrack (26) na Sabato Mwisila (52).
CHANZO ; HABARI LEO.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa