Mkurugenzo mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU
nchini EDWRD HOSEA amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa zaidi ya
shilingi bilioni 39 katika kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi
Disemba mwaka jana kutokana na kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya
rushwa katika idara mbalimbali za serikali.
Mkurugenzi mkuu wa takukuru ameeleza hayo wakati akifungua jengo
jipya la ofisi za taasisi hiyo katika manispaa ya kigoma ujiji, jengo
lililogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.2 ambapo amesema katika
kipindi hicho kesi 256 zilifunguliwa na taasisi hiyo na kwamba
wamejikita zaidi katika kusimamia maadili, ushirikishwaji wa umma na
kuheshimu utawala ambapo ameitaka jamii kuitumia taasisi hiyo
kukabiliana na rushwa katika idara mbalimbali na katika uchaguzi ili
kupata viongozi bora.
Kwa upande wake mkuu wa takukuru mkoa wa kigoma SUZAN RAYMOND na
katibu tawala wa mkoa wa kigoma JOHN NDUNGURU wamesema zaidi ya kesi
sita ziko zinaendelea katika mahakama mbalimbali mkoani kigoma na kwamba
wamejipanga kupambana na vitendo vya rushwa katika kipindi cha uchaguzi
mkuu ujao.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Chanzo :ITV Tanzania
0 comments:
Post a Comment