Home » » DAH, KUNIJUA NDIYO UNANIZINGUA?

DAH, KUNIJUA NDIYO UNANIZINGUA?

Kuna teminoloji moja ya kitasha huwa naizimia sana kutokana na jinsi ilivyokaa kiukweli ingawa ukiicheki kimagumashi inaweza kuwa teminoloji ya kinoko kuliko zote ambazo umewahi kuzisikia mwanangu mwenyewe. Si unajua wenzetu tena faza?
Jamaa unajua anakwambiaje, kitu chochote kile kilichozidi kipimo ni miyeyusho!
..natamani ningeweza kuiweka ile ya kitasha yenyewe lakini najua itazingua tu hapa ukizingatia huku kitaa kuna akina sisi ambao suala la langueji lilikuwa linazingua tangu tuko skonga.
Ndiyo maana ukiibuka kitaani kwangu halafu ukajifanya mtu wa kuwasemesha watu kitasha utamaindiwa.
Unanisemesha kitasha ada ulinilipia au unataka kudistabu tu breini yangu?
Ushazis’kia hizo eh?
Sasa bwana kuna huku kujuana na kutaniana kupitiliza ambako mara nyingi kunatokea kwa washkaji zetu wa kitaa. Longtaimu tulikua tunakip distance ujue, tulikuwa hatutaki mtu atusogelee kwa sana, lakini mida mida hivi tukashtukia kwamba wanetu wa kitaa hawajisikii freshi, wanaanza kuhisi kama wana wakishayapatia wanakichenjia kitaa.
Si unazijua hizo?
Basi sisi tukaamua fresh, ngoja tujimiksi nao, twende sawa lakini bwana tumekuja kugundua kwamba wanetu ukijimiksi nao wanakuwa wanazidiisha zile kuzinguana kimtindo.
Unajua kivipi?
Wanetu wanataka kutuzoea mpaka homu, samtaimz kuna ule utani ambao, unaangalia kwanza mwanangu leo kaongozana na nani? Si unazijua zile au unaangalia kama mwana yuko homu, labda katembelewa na wanawe wa jobu si unaweza kumchunia tu, ukaacha wamalizane na wewe ukaibuka kwa taimu yako?
Siyo hivyo kwa wanetu, mpaka mademu za watu unaambiwa wanawazingua kwa jinsi wanavyotania wana kupitiliza mpaka watu wanafikiria kuanza tena kukipu distansi na kitaa kwa sababu ukikiangalia fresh, ...dizaini kinazingua!
Sasa juzi kati hapa mwanangu, mshkaji flani kumbe jobu kwake ni mtu flani levo za juu, unaona bwana, lakini kitaani kwake akaamua kuishi kawaida tu na wana. Yaani ile akitoka jobu anaibuka skani nini anabonyea na wana mpaka mida mida anaibuka homu.
Mshkaji ana mjengo nini ila bado bachela kwa hiyo samtaimz wana huwa wanaibuka homu, si unazijua zile za kuchoma Mbuzi wikiendi?
..ndiyo zake.
Basi bwana ikatokea akatembelewa na bosi wake siku moja, kumbuka mchizi kazini kwake ni mshua hivi dizaini, wana kwa nini wasiharibu? Wameibuka na maganja nini wanachoma, mwana kila akiwapa ishara kwamba siyo, wana wanakomaa tu wanamwambia asiwazingue.
Unataka kujua kilichotokea mwanangu?
Aliwakanseli tu wana, akawa hataki tena mawasiliano baada ya hapo, yeye na washkaji zake levo za juu tu maana wana wameleta za kujua sana
Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa