Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo
kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga
miundombinu ya umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo wilayani Busega Bw. Steve Thomson (kushoto)
Meneja
wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo
mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani)
Mkazi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega ambaye jina lake halikupatikana mara moja akitoa hoja yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto waliosimama mbele) mara Waziri alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za wananchi
Diwani wa Kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti akielezea
kero za umeme katika kata yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto), viongozi na wananchi (hawapo pichani).
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment