Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kamani, amewaonya
watendaji watakaotafuna fedha za miradi mbalimbali inayotekelezwa
Jimbo la Busega mkoani Simiyu.
Dk. Kamani, alitoa onyo hilo juzi wakati akikagua mradi wa maji
Kijiji cha Nyangili, Kata ya Igalukilo Busega mkoani Simiyu, ambako
pamoja na mambo mengine alikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa
katika kata hiyo.
Alisema mradi huo umetumia fedha nyingi ambazo si bajeti ya serikali,
bali juhudi zake binafsi kama mwakilishi wa wananchi hao,
akiwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo marafiki, wahisani pamoja na
Benki ya Dunia.
“Nawaomba ndugu zangu muulinde mradi huu na kuhakikisha wananchi wanahudumiwa bila kubaguliwa,” alisema.
Mradi huo wa maji katika Kijiji cha Nyangili, umegharimu sh mil. 300 ikiwa ni fedha kutoka Benki ya Dunia.
Dk. Kamani, aliitaja miradi inayotekelezwa Kata ya Igalukilo kuwa ni
pamoja na mradi wa umeme unaopita Kijiji cha Nyangili, Lunala na
Mwamagigisi na mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa kituo cha afya
Igalukilo.
Upande wa ujenzi wa barabara, Dk. Kamani alisema kuwa miradi ya
barabara imetengewa sh mil. 300 ambapo barabara ya Mwamjulila na Badugu
itatengenezwa na itapitika kwa urahisi kuliko ilivyokuwa awali.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment