Home » » WENYEVITI WA VITONGOJI BARIADI WAGOMA.

WENYEVITI WA VITONGOJI BARIADI WAGOMA.

Jiunge na Huduma ya Tone Mobile News Bure kabisa kupitia Whatsapp yako na uwe wa kwanza kupata kile kinachotokea ni Rahisi sana Ingia katika uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika Whatsapp yako kisha andika TONE MOBILE NEWS tuma kwenye namba 0756364660 utapokea ujumbe kuwa umeunganishwa.
 
Na Samwel Mwanga, Simiyu,
 
WENYEVITI  wa Vitongoji katika kata ya Marambo Halmashauri ya Mji wa
Bariadi Mkoani Simiyu wamekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na
serikali kumwajibisha Diwani wa kata hiyo Clementi Matogoro (CCM) kwa
madai ya kutumia ubabe katika kuendesha shughuli za kata hiyo.
 
Mbali na hilo wenyeviti hao wametangaza mgomo wa kutokufanya kazi
yeyote ya maendeleo ndani ya kata hiyo, ikiwa pamoja na kutokushiriki
katika vikao vya maendeleo vya kata (WDCs), ambapo katika kikao cha
maendeleo cha kata kilichofanyika juzi wenyeviti hao walisusia kikao
hicho.
 
Wakiongea na waandishi wa habari katika ofisi za chama cha waandishi
wa habari mkoani hapa mara baada ya kususia kikao hicho, walisema kuwa
hawako tiyari kufanya kazi na diwani huyo kutokana na kuwatukana
pamoja na kuendesha kata kwa ubabe.
 
Walisema kuwa mbali na ubabe pamoja na kutolewa lugha chafu
walimtuhumu diwani huyo kuwa chanzo cha wafanyakazi wa serikali ndani
ya kata hiyo kufukuzwa kazi, na kuamishwa pindi wanapopinga maamuzi
yake.
 
Walibainisha kuwa Matogoro amekuwa akiongea uongo kwa wakuu wa idara
katika halmashauri ya mji ili wafanyakazi hao wafukuzwe kazi au
kuamishwa ndani ya kata yake, ambapo waliodai alisababisha mtendaji wa
kata pamoja na mwalimu mkuu shule ya msingi Bariadi kumishwa na
kushushwa cheo.
 
“Tulikaa kikao cha maendeleo ya kata tarehe 16/04/2014..tukakubalina
kuuza miti kwa wananchi wetu ambayo ilkuwa imekauka katika pori la
marambo..tulipomaliza kikao sisi tulienda kuuza miti hiyo..cha
kushangaza..diwani alitugeuka na kuwakamata wananchi wote ambao
tulikuwa tumewauzia miti hiyo”
 
Alisema John Masunga Mmoja wa wenyeviti hao walisema kuwa mbali na
wananchi hao kukamatwa na kupelekwa kituo cha polisi wilaya diwani
huyo aliwatuhumu viongozi hao kuwa ni wezi kwa kuuza miti hiyo kwa
maslai yao binafsi jambo walilosema kuwa uongo.
 
Alipotafutwa na waandishi wa habari kwenye simu yake diwani huyo
alikataa kuongelea jambo hilo kwa kukata simu alipoulizwa tuhuma hizo
na alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (msg) hakuweza kujibu.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa