Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI wametakiwa kuzilinda na kuzihifadhi Hifadhi za Taifa, ili ziweze kuwa endelevu kwa sababu zina manufaa mengi kwa jamii.
Kauli hiyo ya ilitolewwa mjini hapa juzi na Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kamani, alipokuwa akifungua mradi wa bwawa la
maji katika kitongoji cha Mwabayanda, kilichoko kijiji cha Lamadi,
wilayani Busega mkoani Simiyu.
Alisema bwawa hilo lililochimbwa na Shirika la Hifadhi za Taifa
(Tanapa), kupitia Hifadhi yaTaifa ya Serengeti, ni mkombozi kwa wananchi
hao, kwani litawaondolea kero ya maji iliyodumu kwa muda mrefu.
Alisema kutokana na faida hiyo ya kupata maji kwa ajili ya matumizi
ya binadamu na mifugo, pamoja na miradi mingine, ni vema sasa wananchi
wakazithamini na kuzitunza hifadhi za taifa, ili ziendelee kuwaletea
maendeleo zaidi.
Waziri Kamani ambaye pia ni mbunge wa Busega, aliwataka wananchi
kulitunza bwawa hilo, ili liweze kuwa endelevu, sanjari na kuunda kamati
ya maji itakayosimamia mradi huo.
Pia aliwataka wananchi kuacha kunywesha mifugo yao ndani ya bwawa
hilo na badala yake wazinyweshe kwenye miundombinu iliyowekwa pembezoni.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment