Home » » HOSPITALI YA MEATU HAINA JOKOFU LA KUHIFADHI MAITI.

HOSPITALI YA MEATU HAINA JOKOFU LA KUHIFADHI MAITI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Na Samwel Mwanga,Meatu
 
HOSPITALI ya wilaya Meatu iliyoko katika Mkoa wa Simiyu inakabiliwa na
tatizo la kuharibika kwa Jokofu la kuhifadhia Maiti na hivyo
hulazimika kuzisafirisha na kwenda kuzihifadhi katika Hospitali ya
Wilaya ya Maswa mkoani humo iliyoko umbali wa Kilomita 95 kutoka mjini
Mwanhuzi ambako ndiko makao makuu ya wilaya hiyo.
 
Hali hiyo ambayo imedumu takribani mwezi mmoja sasa imekuwa
ikisababisha usumbufu mkubwa kwa watu wanaofiwa na ndugu zao  katika
hospitali hiyo na hivyo kuamua kuzihifadhi kabla ya taratibu za
mazishi kufanyika.
 
Wakizungumza na Waandishi wa habari mjini Mwanhuzi wananchi hao
walisema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwasababishia majonzi,huzuni na
gharama kubwa za kuhimili misiba huku baadhi ya wafiwa wakiilalamikia
serikali kutochukua hatua za haraka kutatua tatizo hilo kwa kile
walichodai hulazimika kusafiri Umbali mrefu wa kwenda katika Hospitali
ya Wilaya ya Maswa.
 
“Hili ni tatizo hivi karibuni nilifiwa na ndugu yangu aliyekuwa
akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Meatu nililazimika
kusafirisha mwili wa marehemu kilomita 95 hadi mjini Maswa wakati
tukisubiri ndugu na jamaa wa karibu hasa wazazi  waliokuwa wakiishi
Jijiji Dar Es Salaam na kasha kuurejesha kwa ajili ya mazishi kwa
gharama kubwa”Alisema John Madulu.
 
Walisema  kuwa kwa kuzingatia hali halisi ya uchumi na miundo mbinu
ilivyo hivi sasa imekuwa ikiwagharimu wafiwa na hata wengine kujikuta
wakiamua maamuzi yasiyo kuhifadhi ndugu zao kinyume na wosia wao.
 
“Ukweli kuharibika kwa friji ya chumba cha maiti katika hospitali yetu
hapa Mwanhuzi sasa ni tatizo, unakuta umefiwa na unasubiri ndugu
hasawazazi au mke,mume na hata watoto inakuwa vigumu kumudu gharama za
msiba licha ya kuwepo  hatari ya kuharibika kwa mwili wa
marehemu”alisema Juma Shigela.
 
 
Hata hivyo baadhi ya wanannchi hasa waishio vijijini wamekuwa
wakidiriki kuichukua miili ya ndugu na jamaa zao mara tu baada ya
kudungwa sindano za dawa za kuzuia mwili kuharibika haraka.
 
Akizungumzia suala hilo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Meatu Dkt,Saly
Saly alikiri hospitali hiyo kukabiliwa na tatizo hilo  na kuwa uongozi
wa hospitali hiyo umeanza kuchukua hatua madhubutu za kuondoa tatizo
na kero hiyo kwa wananchi wanaohudumiwa na hospitali hiyo.
 
Alisema katika kipindi hiki madaktari wamekuwa wakitumia dawa maalum
za kudunga ili miili ya marehemu isiharibike na kuweza kumudu kuwepo
kwa siku hadi mbili wakisubiri ndugu na jamaa kabla ya kuzika.
 
“ukweli tuna tatizo hilo lakini hatua madhubuti zimeanza kuchukuliwa
na zabuni imetangazwa na mzabuni amepatikana na wakati wowote
tutaondokana na taizo hili, kwani marehemu wetu wamekuwa wakilazimika
kuhifadhiwa hospitali ya mjini Maswa wilayani Maswa kilomita 95 na
kusababsiha usumbufu,huzuni na gharama’alisema Dkt,Saly.
 
Aliongeza kuwa si ndugu na jamaa wote wanaofiwa marehemu wao
wanapelekwa kuhifadhiwa Maswa ni kwa wale wanao hitaji kufanya hivyo
wakati wakisubiri ndugu na jamaa zao kufika kwa ajili ya mazishi.
 
“Hata hivyo baadhi ya ndugu na jamaa wa wafiwa marehemu wao si wote
wanaopeleka marehemu wao hospiatli ya Maswa kwa kuihifadhi,hali hiyo
inajitokeza kwa wale wanaohitaji kufanya hivyo wakati wakisubiri muda
wa siku ya mazishi hasa kwa kusubiriana ndugu na jamaa”alisem Dkt
Saly.
 
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmshauri ya wilaya ya Meatu
Paschal Shindai alisema tayari mzabuni amepatikana kwa ajii ya kununua
jokofu jingine jipya na kuondoa tatizo na kero hiyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa