Na Samwel Mwanga-Busega
HALMASHAURI ya wilaya ya Busega katika mkoa wa Simiyu imemwomba Mkuu
wa wilaya hiyo,Paul Nzindakya kuisaidia kupata kibali kutoka Mamlaka
ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu(SUMATRA)ili waweze kuruhusu magari
ya abiria kuingia katika kituo cha Mabasi cha Lamadi na wao kuweza
kukusanya ushuru.
Ombi hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Charles Lukale
katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi mjini Lamadi
wakati wakizungumzia jinsi ya kukusanya mapato ya ndani.
Alisema kuwa wamekuwa wakipoteza mapato mengi kutokana na magari mengi
ya abiria kutoingia katika kituo cha mabasi cha Lamadi kinachomikiwa
na halmashauri kutokana na kutokuwa na kibali kutoka Sumatra.
“Mkuu wa wilaya tunapata wakati mgumu kuwataka wenye magari
yanayosafirisha abiria kutoingia katika kituo cha mabasi cha Lamadi
kilichoko katika barabara kuu ya Mwanza kwenda Musoma kwani tangu
tuandike barua Sumatra kupata kibali hicho hadi sasa na hasa kutoa
ratiba tu ya magari hayo kupita katika kituo hicho
hatujajibiwa”Alisema
Pia alimuomba Mkuu Wilaya hiyo kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama kuweka kituo cha polisi katika kituo hicho cha
mabasi kwani sehemu yenye mikusanyiko kama hiyo huwa haikosi vurugu
za mara kwa mara.
Aidha alimwomba Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Hamis Yuhan kuangalia
eneo ambalo linafaa kuwa maegesho ya magari makubwa ya kubebea mizigo
kwani hadi sasa jambo hili limekuwa ni kero kwa watumiaji wengine wa
barabara hiyo.
Naye Mkuu wa wilaya hiyo,Mzindakaya aliliagiza jeshi la polisi
wilayani humo kuhakikisha magari yote ya abiria yanayopita mjini
Lamadi kuingia katika kituo hicho cha mabasi ya abiria.
“Naliagiza jeshi la polisi wilayani Busega kuhakikisha kuwa magari
yote ya abiria yanayopita katika mji wa Lamadi kuingia katika kituo
cha mabasi kilichopo mjini hapa ili halmashauri iweze kukusanya mapato
yake ya ndani ambayo yatatumika kuendeleza shughuli za maendeleo
katika wilaya yetu ambayo bado ni mpya na suala la Sumatra
nawahakikishia nitalishughulikia mara moja”
Simiyu yetu Blog
Home »
» HALMASHAURI YA BUSEGA YALIA NA SUMATRA KUIKOSESHA MAPATO.
HALMASHAURI YA BUSEGA YALIA NA SUMATRA KUIKOSESHA MAPATO.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment