Home » » WANAUME ZAIDI YA 18,000 WAFANYIWA TOHARA WILAYANI MEATU

WANAUME ZAIDI YA 18,000 WAFANYIWA TOHARA WILAYANI MEATU

Zaidi wa wanaume 18,146 wilayani Meatu Mkoani Simiyu wamepatiwa tohara katika kampeni iliyofanyika desemba mwaka 2013.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya  John Wanga, amesema hayo leo wakati akizungumza na madiwani na watendaji mbalimbali wlayani humo.

Amesema hali hiyo inalenga kuwakomboa wanaume kuondokana na magonjwa ya ukimwi na zinaa.

Amesema kampeni hiyo itaendelea katika kufanyika katika maeneo mbalimbali wilayani humo yakiwemo ya vijijini.

Kampeni hiyo ilifanyika katika maeneo na vituo 8 vya afya  vya nghoboko, kisesa,mwandoya, mwanhuzi,mwamalole,bukundi,sengwa na sakasaka.

kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukmwi wilayani hapa Basu Kayungiro amewaomba hata wanaume wenye umri mkubwa kujitokeza katika kupata huduma ya tohara.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa