MKUU WA WILAYA YA MASWA ACHOCHEA MOTO
*Wananchi wasema naye amegeuka kuwa mlalamikaji
Na Samwel Mwanga-Maswa
HOTUBA ya Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu,Luteni mstaafu Abdalah
Kihato aliyoitoa juzi katika ufunguzi wa kikao cha baraza la madiwani
wa halmashauri ya wilaya hiyo imechochea moto kwa wananchi wa wilaya
hiyo baada ya kuonyesha kuwalalamikia watendaji wanaodaiwa kuhusika na
vitendo vya kifisadi huku akidaiwa kuwakumbatia viongozi
waliokataliwa wilayani humo .
Viongozi waliokataliwa katika wilaya hiyo mbele ya Naibu Waziri wa
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Aggrey Mwanri kutokana
na kushindwa kuendesha halmashauri ya wilaya hiyo ni Mwenyekiti wa
halmashauri,Stephen Dwese na Mkurugenzi ,Hilda Lauwo.
Wananchi na Wanasiasa waliozungumza na Tanzania daima jana walisema
Mkuu wa wilaya ameungana na wananchi wa kawaida wilayani humo na kuwa
mlalamikaji, badala ya kutoa mwongozo wa nini cha kufanya kuondokana
na suala hilo na kueleza jinsi ya kulikabili genge la watu hao
wanaotafuna fedha ndani ya halmashauri ya Maswa.
Miongoni mwa waliozungumzia hotuba hiyo ni Mwenyekiti wa Chadema wa
baraza la vijana (BAVICHA) wilayani humo,Peter Shiwa alisema kuwa
hotuba ya Kihato ilipaswa kujikita katika kuzungumzia masuala
yanayoikabili wilaya hiyo kwa upana wake na siyo kuvishambulia vyombo
vya habari vinavyoibua uozo ndani ya wilaya hiyo.
Alisema mathalani badala ya kuzungumzia utendaji wa vyombo vya habari
juu ya kuibua matatizo ya wananchi wa wilaya hiyo alipaswa kuwaeleza
wananchi kupitia kikao hicho kuwa serikali ya wilaya imejipangaje
kukabiliana na genge la watu wachache walioteka mamlaka ya wilaya hiyo
na kujichotea mamilioni ya fedha bila kushughulikiwa.
"Kwangu mimi issue si jinsi vyombo vyahabari vinavyofanya kazi
wilayani humo bali kinachoniumiza ni ufisadi ambao ni dalili ya
ugonjwa mzito unaolikabili taifa,ugonjwa wa kutowajibika, kikundi cha
watu wachache kujilimbikizia mali, mfumo wa sheria kutofanya kazi,
tatizo la watendaji ndani ya halmashauri kufanya mambo wanavyotaka,
watu wanachukua posho hata hawajazifanyia kazi wananchi wa Maswa
wanataka majibu ya maswali hayo'Alisema kwa uchungu.
Walisema badala ya kuzungumzia watu tena kwa mafumbo kwa sababu
vyombo vya habari vimeshaandika juu ya watendaji mizigo ndani ya
halmashauri ya wilaya ya Maswa basi DC alipaswa kuzungumzia bigger
picture (mtazamo mpana) si smaller picture, juu ya matatizo ya wilaya
yetu angetuhakikishia namna gani serikali yake ya wilaya imejipanga
katika mapambano dhidi ya ufisadi na siyo kupiga maneno maneno.
Walisema kuwa DC Kihato hawezi kuepuka mzigo wa tuhuma dhidi ya
viongozi wabovu wilayani humo kwani amekuwa mstari wa mbele kuwatetea
kwa maslahi binafsi pia anapaswa kuwaeleza Wana Maswa jinsi
alivyoshindwa kuongoza wilaya hiyo na kubaki kulalamika.
"DC hapaswi kulalamika kama anavyolalamika mwananchi wa kawaida katika
hotuba ya juzi amekiri kuwa wapo watu waliokwapua shilingi milioni 20
kama ana ushahidi wa kutosha angeagiza vyombo vya sheria kuchunguza
suala hilo na wahusika wafikishwe mahakamani na siyo kulalamika tu
tena kwa mafumbo huko ni kuonyesha udhaifu katika uongozi wake
"alisema Joseph John.
Walisema kuwa wanasikitishwa na kitendo cha Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo,Stephen Dwese kukubali kikao hicho kinachotumia fedha za walipa
kodi wa nchi hii kugeuzwa kama kijiwe cha mipasho kwani sehemu kubwa
ya hotuba hiyo ilijaa kejeri,matusi na mafumbo hali ambayo
imelishushia heshima baraza hilo.
'baraza la madiwani la Maswa kwa sasa limekosa heshima maana
linageuzwa kuwa kijiwe cha mipasho kutokana na kuruhusiwa kuwepo kwa
vitendo vya kejeri,matusi na mafumbo
vilivyofanywa wazi na Mkuu wa wilaya huo ni udhaifu wa mwenyekiti wa
halmashauri Mh Dwese kwani hicho si kikao cha DC kwa nini aendelee
kuporomosha matusi naye yupo hapo mezani anachekacheka tu hilo baraza
lina heshima yake ndilo linaloamua mambo ya wananchi wa wilaya
kisigeuzwe kama kijiwe cha mitaani "alisema kwa hasira Sulu Machibya.
Hata hivyo wananchi hao walivitaka vyombo vya habari kutokurudi nyuma
katika utendaji wa kazi zao huku wakiwabeza watu wanaotumia muda wao
kuwatisha waandishi wa habari wanaoibua tuhuma dhidi yao huku
wakisisitiza kuwa vyombo vya habari ndiyo sauti ya wananchi..
"vyombo vya habari chapeni kazi kwa maana siye tunaamini habari
mnazoandika au kuzitangaza zina ukweli na usahihi hivyo msiwasikilize
watu wachache wanaowatisha tisha hizo ni changamoto za kazi kumbukeni
utelezi wa mlenda haumwangushi mtu mzima kwani malalamiko
mnayoyaandika au kuyatangaza yanatoka kwetu sisi wananchi ambao
tunanyanyasika au tunaona yana kwenda ndivyo sivyo na mmekuwa msaada
mkubwa sana kwa wananchi"alisema Eva Charles.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment