Home »
» Wakulima wa pamba waigeuzia kibao serikali
Wakulima wa pamba waigeuzia kibao serikali
Baadhi
ya wakulima wa zao la pamba mkoani Simiyu wameanza kukusanya saini zao
kwa lengo la kuwasilisha rasmi madai yao mbele ya Serikali na Bodi ya
Pamba nchini (TCB) ili waweze kulipwa fi dia kutokana na kuuziwa mbegu
ambazo zimegoma kuota.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa
waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita na Mwenyekiti wa Chama
cha Wakulima wa Pamba nchini (TACOGA), Elias Zizi alisema hivi sasa
wanaendelea kukusanya saini hizo katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu
na baadaye wataendelea katika wilaya nyingine.
Alisema lengo la
kukusanywa kwa saini hizo kutoka kwa wakulima mbalimbali ni kutaka
kuwasilisha rasmi madai yao serikalini kuitaka
Kampuni ya Quton
iliyopewa kazi ya kuwauzia mbegu za pamba katika msimu wa mwaka huu
iweze kuwalipa fidia baada ya mbegu walizouziwa kushindwa kuota na
kuwasababishia hasara kubwa.
" Kwa kweli wakulima wamechukizwa na kitendo cha kuuziwa mbegu ambazo zimegoma
kuota
pamoja na kupigiwa debe na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo
wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na watendaji wetu wa bodi ya pamba,"
"Walishinikiza kupandwa kwa mbegu hizo zisizo na manyoya kwa madai ndizo zenye ubora na
uhakika
wa kuota kwa asilimia 90 ikilinganishwa na zile zenye manyoya ambazo
kwa kipindi kirefu ndizo tumekuwa tukipanda na kuota pasipo matatizo,
lakini hali imekuwa tofauti, sasa lazima tulipwe fidia," alisema Zizi.
Mwenyekiti huyo alisema wakulima wa zao la pamba wamechoka kila mwaka kuyumbishwa na watendaji wa Serikali ambapo chombo
kilichokabidhiwa
dhamana ya kuwasaidia (Bodi ya Pamba) kimeshindwa kutimiza wajibu wake
na badala yake hivi sasa kinawasaidia zaidi wanunuzi wa zao hilo.
Alisema
baada ya kukamilika kwa kazi ya kukusanya saini hatua itakayofuata
itakuwa ni kuwasiliana na wanasheria ili kuwezesha kuyaweka madai yao
kisheria zaidi ili wale wote walionunua mbegu zinazosambazwa na Quton na
zikagoma kuota waweze kulipwa fidia.
Serikali miaka mitatu nyuma tuliiona jinsi ilivyohangaika kuwalipa fidia wenzetu wenye
kampuni
zinazonunua pamba baada ya uchumi wa dunia kuyumba,wengi walilipwa fi
dia ya mamilioni ya shilingi, itakuwa ni ajabu kwa Serikali ikatae
kuielekeza kampuni ya Quton ili iweze kutulipa fidia, alisema Zizi.
Al
i s ema , awa l i wa k a t i viongozi wa Serikali na bodi ya pamba
wakihimiza matumizi ya mbegu hizo za Quton wakulima walihoji utofauti na
ubora wake unasababishwa na kitu gani kwa
vile mbegu hiyo ni ile ile ya UK.91 iliyozoeleka kwa kipindi kirefu na kwamba iweje itolewe tu manyoya ndiyo iwe bora.
Hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko ya wakulima wengi wa zao la pamba katika Mikoa
ya Simiyu, Shinyanga, Geita nabaadhi ya wilaya za Mkoa wa Tabora kulalamikia kitendo cha
kugoma kuota kwa mbegu za pamba zilizosambazwa na Kampuni ya Quton yenye makao yake wilayani Bariadi Mkoa wa Simiy
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment