Wadau wa elimu mkoani
simiyu wamesema kuwa kufanya vibaya kwa shule nyingi za msingi na
sekondari kunachangiwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati.
Hali hiyo imeelezwa
na wadau wa elimu mkoani hapa wakati walipokutana katika kikao cha pamoja
kujadili hali ya elimu mkoani hapa mjini bariadi.
Wamesema kuwa hali
hiyo imekuwa ikichangia kwa kiwango kikubwa shule nyingi kufanya vibaya katika
ufaulu wa mitihani yake.
Wadau hao wamesikitishwa
na kitendo cha shulenyingi kutokuwa na madawati hali ambayo inawalazimu
wanafunzi kuandika kwa ktumia mapaja na wengine kushikilia madaftari mikononi.
Naye kati bu
tawala mkoani hapa bi,mwamvua jilumbi amewataka wadau na watu wengine
kujitokeza kubuni njia za kutatua kero zilizopo katika shule za maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment