Mahakama ya wilaya ya
bariadi mkoani simiyu imewahukumu watu wawili kutumikia kifungo cha miaka 40
jela au kulipa faini mil30 baada ya kupatikana na kosa la kufanya ujagili
katika hifadhi ya taifa ya maswa.
Waliokumbwa na hukumu hiyo ni
Mandago Say (58) na Feya Say (64) wote wakazi wa wilayani meatu mkoani hapa.
Hukumu hiyo imetolewa
na hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo Robart Oguda baada ya kuridhishwa na
ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Awali ilidaiwa na
mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta Samweli Kilabuko kuwa watuhumiwa
walitenda kosa hilo april mwaka huu kwa kuingia katika hifadhi ya taifa ya
maswa na kuwinda bila ya kuwa na kibali.
Na kuwauwa wanyama
wawili ambao ni swala na nyati wakiwa na gharama ya zaidi ya mil 9 kwa
kutumia silaha.
0 comments:
Post a Comment