Mwalimu wa shule ya msingi Mwasengela wilayani Meatu Mkoani Simiyu ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojilikana.
Tukio hilo limetokea katika kijiji na kata ya Mwaswale tarafa ya Bumera wilayani Itilima mkoani hapa.
Kaimu
Kamanda wa Polisi ACP Venance Kimario amemtaja mwalimu huyo kuwa ni
Vicent Mganga (67) ambaye ni wa shule ya msingi mwasengela.
Amesema
aliuawa kwa kupigwa risasi majira ya saa mbili usiku na mtu au watu
wasiojulikana ambao walitoweka mara baada ya kutenda mauji hayo.
kamanda huyo amesema polisi bado inaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na hakuna mtu anayeshikliwa na polisi..
0 comments:
Post a Comment