Home » » MUME AMCHARAZA VIBOKO MKEWE HADI KUMUUA

MUME AMCHARAZA VIBOKO MKEWE HADI KUMUUA

Mwanamke mmoja wilayani maswa mkoani simiyu ameuawa kwa kushambuliwa kwa kupigwa na fimbo na mume wake kutokana na wivu wa kimapenzi.
Tukio hilo limetokea des 15 katika kijiji cha buyubi kata ya buchambi wilayani maswa mkoani hapa.
Kaimu Kamanda Wa Polisi Mkoani Simiyu ACP Venance Kimario amemtaja aliyeuawa kuwa ni Adela Mbugwisha (35) wa kijiji cha buyubi.
Amesema mwanamke huyo aliuawa kwa kushambuliwa kwa kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake niga jionela (37)
Amesema chanzo cha tukio ni wivu wa kimapenzi, na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa