![]() |
Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Erasto Sima, akikagua kikosi cha mgambo wakati akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya Mgambo katika Kijiji cha Ikungulyambeshi ‘A’ Kata ya Kilalo wilayani humo. |
![]() |
Kikosi kikipita kutoa heshima. |
![]() |
"Heshimaaaa....Toaaa....!!" |
![]() |
kwa-kwa-kwa-kwaaa..! |
![]() |
Ukakamavu. |
![]() |
Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Erasto Sima, akihutubia wakati wa shughuli ya kuhitimisha awamu ya kwanza ya mafunzo ya Mgambo katika Kijiji cha Ikungulyambeshi ‘A’ Kata ya Kilalo wilayani humo. |
![]() |
Mshauri wa Mgambo wa wilaya hiyo Sajenti Ndasan Josephat akitoa nasaha zake. |
![]() |
"Ili muwe wakakamavu mwahitaji kuwa na afya na afya hujengwa kwa mazoezi" |
![]() |
Picha ya pamoja. |
SERIKALI wilayani hapa, imewaagiza vijana waliohitimu mafunzo ya
Mgambo wasaidie kukamata wahalifu mbalimbali, wakiwemo wahamiaji haramu
waliokimbia opalesheni Kimbunga na kujificha wilayani humo.
Imewaonya baadhi ya wanasiasa wanaopinga mafunzo hayo na kuwaasa vijana
hao wasitumie vibaya mafunzo waliyopata, yakiwemo ya siraha, kwa
kujihusisha na vitendo vya ujambazi, ujangiri, uuzaji na utumiaji wa
madawa ya kulevya, vinginevyo watakiona cha mtema kuni.
Wito huo ulitolena na Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Erasto Sima, juzi
katika Kijiji cha Ikungulyambeshi ‘A’ Kata ya Kilalo wilayani humo,
wakati akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya Mgambo Katani humo.
Sima alisema kwamba, baadhi ya watu wakiwemo wana siasa walijaribu
kukwamisha mafunzo hayo kwa kuwashawishi vijana wasishiriki lakini
wananchi na viongozi wanaojali maslahi ya umma, walisimama kidete na
kushirikiana na wakufunzi wa JWTZ, hatimaye mafunzo hayo yakafanyika kwa
ufanisi.
“Baadhi waliona mafunzo haya ni jambo la kisiasa wakati sivyo, maafunzo
haya ni kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi yetu hivyo mliopata
mafunzo, msaidie opaleshen Kimbunga kwa kufichua wahamiaji haramu
waliokimbilia kujificha huku.” Alisema Mkuu huyo.
Alieleza kuwa ni wajibu wao kulisaidia taifa kupambana na uhalifu
mbalimbali ukiwemo dawa za kulevya, rushwa, majambazi, majangiri ambayo
yanaisumbua nchi yetu na kujitolea katika shughuli mbalimbali za ujenzi
wa taifa.
“Jeshi la Mgambo limeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 147, kifungu (1) na (2) kwa
kuwa vijana ndiyo tegemeo la taifa, msikub ali kushawishiwa kukataa
mafunzo ya mgambo, wanaowakataza ni maadui wa ndani wasioitakia mema
Tanzania, ole wao watakao bainika.” Alionya Sima.
Mshauri wa Mgambo wa wilaya hiyo Sajenti Ndasan Josephat akiwapongeza
vijana hao na wakufunzi wa JWTZ, alieleza kwamba, anayo furaha kubwa
kupata walinzi 138 waliohitimu mafunzo ya ukakamavu, ujanja wa porini,
mbinu za kivita na siraha ndogondogo kwa manufaa ya umaa.
Awali katika risara yao iliyosomwa na Hosea Peter, Mgambo hao walisema
kwamba walioandikishwa katika mafunzo hayo walikuwa vijana 540 lakini
waliohitimu ni 138 ( wanawake wakiwa sita) kutokana na wengine kukimbia
mafunzo hayo kwa kushawishiwa na baadhi ya watu.
Vijana hao waliiomba serikali iwape kipaumbele katika nafasi mbalimbali
za ulinzi zinazopatikana na kuahidi kufanya kazi za kujitolea kulinda
usalama wa wananchi na mali zao pia kupambana na kila aina ya uhaifu
katika maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment