Katika hali isiyo ya
kawaida, Mbunge wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu, Bw. John Shibuda,
juzi alijikuta katika wakati mgumu baada ya kupigiwa kura za kumtaka
atoke nje ya ukumbi wa mkutano ambao uliandaliwa na Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), kwa lengo la kuchagua viongozi wa Kanda ya Ziwa
Mashariki akidaiwa ni msaliti.
Hali hiyo ilitokana na hoja
iliyotolewa na mjumbe mmoja ndani ya kikao hicho ambacho kilifanyika
Mjini Shinyanga kikiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Bw.Freeman
Mbowe.
Mjumbe huyo alisimama na kuomba Bw .Shibuda atolewe nje ya
kikao akidai haaminiki na mara nyingi amekuwa akitoa siri za chama hicho
kwa viongozi wa CCM.
Hatua ya kutimuliwa kwa Shibuda ilikuja muda
mfupi baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA kufungua kikao hicho
ambapo mjumbe huyo kutoka Mwibara Bunda mkoani Mara, Ahmed Nkunda
alisimama na kutoa hoja yake lakini hata hivyo Shibuda aliamua yeye
mwenyewe kutoka ili kuepusha vurugu.
Kitendo cha kutolewa nje Bw.
Shibuda,kilisababisha kundi kubwa la wajum be wengine kumfuata
wakionesha wazi kutounga mkono hoja ya mjumbe mwenzao na ku onesha
mpasuko wa wazi ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Hata
hivyo, kabla ya Bw. Shibuda hajatoka nje, Bw, Mbowe alimuomba asitoke
ndani ya kikao hadi awahoji wajumbe wengine kam a wanaafiki hoja hiyo
ili kujua ni wangapi wanaunga mkon o na wangapi wanataka aendelee
kuwepo.
Matokeo ya kura hizo yalionesha wajumbe 90 waliunga mkono
aondoke ndani ya kikao na 30 wakitaka aendelee kubaki ambapo baadhi y a
wajumbe walisema,Bw. Mbowe alishindwa kusimamia mchakato huo kwani se
hemu kubwa ya wajumbe waliotaka Bw. Shibuda abaki hawakuhesabiwa.
Mmoja
wa wajumbe waliotaka mbunge huyo ab aki(jina tunalo ), alisema
uhesabuji kura uliofa nywa na Bw. Mbowe haukuwa sahihi kwani kura hizo
ziliegemea upande mmoja ndiyo sa babu ambayo ilichangia wajumbe wengine
kuon doka ndani ya ukumbi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Bw.S hibuda alidai kusikitishwa na kitendo cha kutole wa nje ya kikao
kwa kupigiwa kura wakati yeye mwenyewe alishaafiki kutoka nje kwa hiari
yake ili kuepusha kuvurugika kwa kikao hicho.
“Kilichoniponza hadi
nionekane msaliti ndan i ya chama ni kitendo changu cha kuwatetea
wakulima wa zao la pamba na wafugaji katika jimbo langu. ..hivi karibuni
nilifikisha kilio chao kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Abdulrahman Kinana.
“Mimi si msaliti kwa kile nilichokifanya bali natetea hakina
masilahi ya wapiga kura wangu, wakulima na wafugaji, pale Meatu
nilipanda katika jukwaa la CCM kumweleza Kinana matati zo ya wapiga kura
wangu maana yeye ndiye mwenye Serikali iliyoko madarakani kwa
sasa,”alisema Bw. Shibuda.
Aliongeza kuwa, hakuna njia ya mkato ya
wananchi kutatuliwa kero zao bila ya kupitia chama tawala ambapo
wakulima wa pamba na wafugaji, wanahitaji tiba badala ya maneno m atupu
ya ukuwadi na uwakala wa kuwa pumbaza kisiasa hivyo utatuzi wa matatizo
yao ni Serikali ya CCM iliyoko madarakani.
Bw.Shibuda alisema
utetezi wake kwa wapig a kura umemfanya aonekane msaliti,Bw. Mbowe
aliwahi kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kazi nzuri ya kuwapelekea
maendeleo wananchi wa jimbo lake sasa kwa nini asionekane msaliti.
“Kwangu
mimi,masilahi ya wafugaji na wakulima wa zao la pamba ndiyo kipaum bele
changu cha siasa za uokovu na ukombozi, kama ingebidi kwenda kwa
shetani kutafuta tiba ya matatizo yao hakika ningekwenda achilia mbali
CCM, kwa sasa chama tawala ndiyo chenye tiba hatuwezi kuwakwepa,”
alisema Bw. Shibuda
CHANZO;MAJIRA
0 comments:
Post a Comment