Home »
» Bariadi waanzisha operesheni saka vyoo
Bariadi waanzisha operesheni saka vyoo
|
|
SERIKALI wilayani Bariadi, mkoani Simiyu, imetangaza operesheni maalumu kwa ajili ya kusaka familia zisizokuwa na vyoo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kugundulika kuwepo kwa familia nyingi
hasa za vijijini kutokuwa na huduma hiyo, jambo linalohatarisha kuzuka
kwa magonjwa ya mlipuko na uchafuzi wa mazingira.
Operesheni hiyo ilitangazwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Erasto
Sima, alipozungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmshauri
hiyo.
Alisema operesheni hiyo imelenga kuiwezesha jamii kuchimba vyoo vya
kudumu, ili kuepukana na maradhi yanayoweza kuwakumba wananchi, na
itaanza muda wowote kuanzia sasa.
“Imegundulika familia nyingi hasa zile za vijijini hapa Bariadi
hazina kabisa vyoo. Watu na familia zao wanajisaidia vichakani,”
alisema.
Alisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya familia
zitakazobainika kutokuwa na vyoo, hivyo kuwataka wananchi kuhakikisha
wanakuwa na vyoo majumbani mwao.
Pia aliwataka madiwani kuwataarifu wananchi wao kabla ya kuanza kwa
msako huo, utakaokwenda kaya kwa kaya, kitongoji kwa kitongoji na
kijiji kwa kijiji.
Chanzo;Tanzania Daima
|
|
0 comments:
Post a Comment