Na mtaalam kutoka Simiyu
Ikiwa
ni mara yako ya kwanza kusafiri kwa ndege unaweza kuona ugumu na pengine kuwa
na shaka juu ya usafiri wa anga kutokana na kukosa taarifa za kutosha.
Nalazimika
kutoa maelekezo haya kwa sababu ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayeweza
kukupatia wakati wa safari yako hasa kutokana na watu wengi utakaokutana nao
kwenye ndege kuwa na uzoefu wa kusafiri mara kwa mara na kufikiri kila aliyemo
ndani naye ni mzoefu.
Mambo
ya muhimu kuzingatia wakati unapanga kusafiri kwa ndege ni pamoja na wakati wa
kukata tiketi, wakati wa kupaki mizigo yako, nini cha kufanya unapofika uwanja
wa ndege, uende wapi, vitu vya kuzingatia wakati wa safari, nanma ya
kushughulikia uunganishaji wa safari (kama unasafiri masafa marefu na unahitaji
kuunganisha ndege nyingine), wapi pa kuchukua mizigo yako ukifika uendako na
kujua swala la usalama wako na mizigo yako.
Wala
hupaswi kupaniki, japo kuwa kusafiri kwa ndege kunaweza kukuchanganya kwa mara
ya kwanza lakini ukishakuwa mzoefu utaona kila kitu mteremko na kuenjoy safari
zako zote.
Sasa
wengi wetu huwa hatutaki kujulikana kama ni ma-first time flyers kwa kuogopa
kuchekwa, lakini tambua kuwa kila unayemuona kwenye ndege inaweza kuwa ni mara
yake ya kwanza kusafiri na ndege hata kama sio lakini naye alikuwa first time
flyer wakati anaanza kutumia usafiri huo, kwa hiyo usisite kuuliza wahudumu au
hata msafiri mwenzako kwa msaada zaidi.
Baada
ya utangulizi huo sasa tuyaone maeneo muhimu wakati wa safari yako ya ndege;
Tiketi; Kuna aina mbili za tiketi za ndege, tiketi za mtandao za elektroniki (e-ticket) na zile tiketi za kawaida (traditional tickets) hata hivyo mashirika mengi ya ndege siku hzi yanatoa sana tiketi za mtandaoni kutoka na kuwepo mfumo wa kulipa kwa njia ya mtandao.
Ili kupata
ticketi yako unatakiwa kuwa na kitambulisho kama vile, leseni ya udereva, kadi
ya mpiga kura (kwa wasafiri wa ndani ya nchi) na pasi ya kusafiria (passport
kwa wasafiri wanaosafiri nje ya nchi). Njia za kufanya malipo ya tiketi yako ni
pamoja na kadi za benki (visa card and master card), kwa Tanzania pia unaweza
kulipa kwa kutumia M-pesa, Tigo-Pesa, Airtel-Money na Ezzy Money.
Unachopaswa kujua wakati unakata tiketi
Kuna aina tatu ya madaraja ya tiketi; Economy, Business na First Class na hata haya madaraja pia yamegawanyika kwa namna yake lakini kukibwa ni kwamba kila daraja lina gharama zake kulingana na huduma zinazotolewa kwa abiria akiwa safarini.
Economy; hili ni daraja la chini na hivyo gharama zake za nauli ni ndogo na mara nyingi huduma zake ndani ya ndege zinajumuisha vitu vichache pia
Business and First Class; Haya ni madaraja ya juu ambayo gharama zake za nauli ni kubwa na huduma zake ni nzuri zaidi kwa abiria, ni vizuri kuuliza ni mambo gani utapata ukikata tiketi ya aina hii ili kuona uhalali wa pesa yako.
Una mahitaji maalumu?
Endapo wewe ni
mlemvu, unasafiri na watoto na nk, inashauriwa kutoa taarifa hizi wakati
ukikata tiketi ili usije kupata shida wakati wa safari yako ukifika.
Unahitaji Chakula maalumu?
Kama tiketi
yako inaonyesha kuwa utapata na chakula wakati wa safari yako unahitaji kutoa
taarifa ya aina ya chakula unachokula, maana kuna wengine hawali nyama
(vegiterians) toa taarifa hizo wakati ukifanya booking ya tiketi yako. Zingatia
kuwa sio kila ndge hutoa huduma ya chakula mashirika mengine hayafanyi hivyo.
Unapenda kukaa siti ya dirishani?
Ni kawaida
unaweza kuchagua nafasi ya dirishani (kama kuna nafasi), mara nyingi mashirika
mengi ya ndege hukupa nafasi ya kuchagua siti wakati wa kukata tiketi yako.
Siti za dirishani ni nzuri sana kwa watu wanaosafiri kwa mara ya kwanza kwa
maana huwapa fursa ya kuona nje ya ndege lakini wale watu warefu sana ni vyema
kukata tiketi ya kwenye korido ili waweze kukaa vizuri.
Ratiba
Iwe unanuanua
tiketi yako kwenye ofisi moja kwa moja au kwa njia ya mtandao, omba kupatiwa
ratiba ya safari yako, kuna taarifa ndogo lakini muhimu ambazo watu huwa
wanajisahau na baade kukutwa na majanga, lazima ujue, ndege inaondokea uwanja
gani, muda, reservation number, uunganishaji wa ndege, na kadhalika (mara
nyingi e-tickets inakuwa na taarifa hizi zote hivyo ni vizuri kuisoma).
Itaendelea………..
Chanzo: tabianchiblog
0 comments:
Post a Comment