Home » » POLISI SIMIYU YATAFUTA MWAROBAINI YA UHALIFU

POLISI SIMIYU YATAFUTA MWAROBAINI YA UHALIFU

JESHI la Polisi Mkoani Simyu limeweka mikakati mbalimbali katika kupambana na vitendo vya uharifu.
.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Sallum  Msangi amesema mikakati hiyo imewekwa ili kupambana na vitendo vya uharifu na mauaji vinavyotokea mkoani hapa.

Mikakati hiyo ni kuishinikiza jamii iwe na mwamko wa kutoa ushirikiano katika  kubaini vitendo viovu miongoni mwa watu wanaowashuku.

Utekelezwaji wa falsa ya jamii kuweza kuwabaini na wafichua waharifu ikiwemo wanaojihusisha na wauaji na biashara haramu za madawa ya kulevya.

Amesema amekuwa akipita maeneo yote yaliyo ndani ya Mkoa kwa kuielekeza jamii namna ya kuwatambua  na kuwabaini waharifu.

Tayari waendesha pikipiki maarufu Bodaboda Elfu 1000  mkoani hapa wamepatiwa mafunzo hayo na kupatiwa vyeti na jeshi la polisi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa