ZAIDI ya watu 92 katika kata ya Badi wilayani
Maswa wamekosa mahali pa kuishi kufuatia nyumba zao kuaribiwa na mvua
zinazoendelea kunyesha.
Mtendaji wa kata hiyo Gervas Nywage,amesema
uharibifu huo umetokea katika vijiji vya Muhida na Jihu kwa nyakati tofauti
katani humo.
Amesema katika uharibifu huo zaidi ya nyumba
102 zikiwemo zilizoezekwa kwa nyasi 44 zimearibiwa na mvua iliyoambatana na
mafuriko.
Mtendaji huyo amesema katika uharibifu huo yamo
mashamba ya mazao na vyakula ikiwemo miundominu ya barabara.
Naye Diwani wa Kata hiyo Bw Martine Masele ameiomba
serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa kuwapelekea wahanga hao
misaada ikiwemo vyakula.
0 comments:
Post a Comment