na Samwel Mwanga, Maswa
MKAZI wa kijiji
cha Isulilo katika wilaya ya Maswa, ameuawa na kisha mwili wake kuchomwa moto
baada ya kumbaka mtoto wa miaka sita.
Taarifa
zilizopatikana kijijini hapo na kuthibitishwa na ofisa mtendaji wa kata ya
Isanga, Charles Nghubuyabano, zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira
ya saa 3:00 asubuhi.
Kijana
aliyeuawa alitajwa kuwa ni Ndaki Ndaki (25) ambaye alikuwa akifanya kazi ya
kuchunga mifugo kijijini hapo akitokea katika wilaya ya Bariadi.
Nghubuyabano
alisema kuwa siku ya tukio, Ndaki akiwa katika kazi yake hiyo, alimwona mtoto
huyo na kisha kumkamata na kuanza kumbaka katika moja ya vichaka vilivyokuwa
karibu na eneo hilo.
“Wakati
akiendelea na unyama wake huo, mtoto huyo alikuwa akilia kutokana na maumivu
aliyoyapata kwani kitendo hicho kilimsababishia kutoka damu nyingi sehemu za
siri na hivyo kuamua kumnyonga na kumuua ili kupoteza ushahidi,” alisema.
Baada ya
kumaliza unyama wake huo baadhi ya watu waliosikia sauti ya mtoto, walianza
kufuatilia kujua ni kitu gani kilichomsibu ndipo walipomkuta Ndaki akijaribu
kuuhifadhi kichakani mwili huo.
Baada ya
kugundua kuwa amejulikana aliamua kukimbia lakini alikamatwa na alipohojiwa
alikiri kubaka na kisha kuua na hivyo wananchi hao walianza kumshambulia kwa
kumpiga kwa kutumia mawe na silaha za jadi hadi alipopoteza maisha na kisha
kuuchoma mwili wake kwa moto.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Salum Msangi, alikiri
kutokea kwa tuki hilo na kuwaomba wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria
mikononi.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment