Na Mwandishi wetu, Bariadi
SERIKALI imesema haiwezi kuongeza bei ya zao la Pamba nchini kwa vile bei ya hiyo inategemea hitaji na mabadiliko katika soko la dunia. Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Bariadi mkoani Simiyu na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, wakati akizungumza na viongozi na wananchi wa vijiji vya Ibulyu na Isanga.
Wassira alisema wingi wa Pamba katika soko la dunia msimu huu umechangia kuporomosha bei ya zao hilo kwa kiasi kikubwa kinyume na matarajio ya wakulima.
Alisema wakulima walilima zao hilo kwa wingi msimu huu wakitarajia wengeweza kuuza kilo moja kwa Sh 1000 na kuendelea lakini hali imekuwa tofauti.
Wassira aliwataka viongozi hao kwenda kwa wakulima vijijini ili kuondoa dhana ambayo imekuwa ikijitokeza kuwa Serikali inahusika na kupanga ama kushusha bei ya zao hilo.
“Hili la Pamba wapo wanaopita wanasema Serikali imeshusha bei, ni lini Serikali ya Tanzania ilipanga bei ya Pamba katika soko la dunia?
“Serikali haipangi bei wala kushusha, hiyo ni kazi ya soko la dunia, ni sawa na mfugaji, ukipeleka ng’ombe mnadani ukakukuta ng’ombe ni wengi lazima utauza kwa bei ya chini,”alisema.
Kutokana na hali hiyo, Wassira alisema baada ya bei hiyo kushuka, Serikali imelazimika kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha inampunguzia mzigo mkulima.
Hiyo ni pamoja na kupunguza ushuru wa asilimia 3 uliokuwa ukitozwa na Serikali za Mitaa ili kuongeza katika bei ya 525 iliyopangwa na wanunuzi hadi kufikia Sh 660 ambayo inalipwa kwa kilo moja kwa sasa.
Hata hivyo waziri huyo alisema, ili kuondokana na tatizo hilo, lisiathiri zaidi wakulima, Serikali inawahimiza wamiliki wa vinu vya kuchambua Pamba na viwanda vya nguo kufikiria kuzalisha nyuzi na nguo.
“Tukiacha kupeleka nje pamba ghafi baada ya kuondoa mbegu tuanze sasa kutengeneza nyuzi na nguo tukifanya hivyo hata kama bei itayumba katika soko la dunia sisi hatutaathirika,”aliongeza.
Hivi sasa wakulima wa Pamba nchini wanalazimika kuuza kilo moja ya Pamba kwa Sh 660, ikiwa ni baada ya Serikali kuongeza Sh 125 kwa kila kilo moja ili kufidia hasara ambayo ingeweza kuwapata wakulima.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment