Mwandishi wetu, Meatu
SERIKALI imetoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya fidia ya ng’ombe 22 wanaodaiwa kuuwa kwa kupigwa risasi na askari wa wanyamapori katika pori la akiba la Maswa mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa maliasili na utalii Mhe Lazaro Nyalandu amesema lengo ni kurejesha mahusiano mazuri baina ya askari wa wanyamapori na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo kutokana na uhasama ulioanza kujitokeza baada kuuawa kwa mifugo hiyo.
Akizungumza na baadhi ya wananchi wanaozunguka pori hilo jana, Mhe Nyalandu amesema wakati taarifa ya tume iliyoundwa kuchunguza mgogoro huo ikiendelea kusubiriwa, serikali imeamua kutoa fidia kwa ng’ombe 22 wanaodaiwa kuuwa kwa kupigwa risasi.
Hata hivyo amewataka wananchi kuzingatia sheria kwa kutoingiza mifugo kwenye pori hilo la akiba
Tangu kuzuka kwa mgogoro huo mwaka 2005, watu sita wakiwemo askari wa wanyamapori wameuawa huku wafugaji kukitozwa faini ya shilingi 72 kwa kuchungia kwenye pori hilo mwaka uliopita.
0 comments:
Post a Comment