Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
MKUU
wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amewata Viongozi wa Dini na Watanzania
kuendelea kumuombea Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za
kurejesha misingi ya maadili, nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa
umma iliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.
Anasema
katika kipindi cha mwaka mmoja wa Utawala wa Rais John Pombe Magufuli,
Serikali ya Awamu ya tano imejipambanua kwa vitendo katika kupiga vita
rushwa, ufisadi na kusimamia nidhamu na miiko ya Uongozi katika utumishi
wa Umma.
Hayo
yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony
Mtaka wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi kuelekea
katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara.
“Ndani
ya Rais Magufuli anaonekana, Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mstari wa
mbele katika kukemea hadharani vitendo vya uvunjifu wa maadili ya
mtumishi wa umma ikiwemo rushwa na ufisadi” anasema Mtaka.
Kwa
mujibu wa Mtaka anasema hatua zinazoendelea kuchuliwa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli katika kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma ikiwemo
mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ni jambo la kupongezwa, kwa kuwa
limelenga katika kuwakumbusha watendaji kuwa Uongozi ni dhamana.
Alisema
kuwa hatua zinazochuliwa na Rais John Pombe Magufuli, zinaendelea
kuongeza heshima ya Viongozi wa Tanzania katika medani ya kimataifa ya
kusimamia nidhamu, maadili na miiko ya Uongozi ambayo imetekelezwa
katika kipindi chote cha miaka 55 ya uhuru.
Anaongeza
kuwa, hatua hizo zilizofikiwa na Viongozi hao ni changamoto kwa
Viongozi Vijana waliopo nchini kuendelea kuheshimu misingi iliyoachwa na
waasisi wa taifa, na hivyo kuiwezesha Tanzania kuendelea kupiga hatua
kubwa za maendeleo katika siku za usoni.
Mtaka
alisema Kiongozi wa Umma ni kioo na kiunganishi katika jamii
anayoiongoza, hivyo ni wajibu wa kila kiongozi wa umma kujenga taswira
chanya ya kiutawala katika kuwahudumia wananchi kwa kutambua kuwa
dhamana ya kiongozi ndio tumaini la watawaliwa.
“Katika
siku za hivi karibuni tumeshudia sekta binafsi zikichukua watumishi
waaandamizi kutoka Serikalini, hiki ni kiashiria kuwa nidhamu na maadili
ya kazi yameimarika kwa kiasi kikubwa sana Serikalini” alisema Mtaka.
Akifafanua
zaidi Mtaka alisema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu
ya Awamu ya tano pamekuwepo na mageuzi makubwa katika utendaji na uwazi
wa shughuli mbalimbali za Serikali, hatua iliyosaidia kuokoa kiasi
kikubwa cha fedha kilichokuwa kikipotea katika miaka ya nyuma.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment