Mwalimu Pendo akipata matibabu
MWANAFUNZI
Marco Limbe(14) aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya
msingi Yitwimila iliyoko kata ya Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu
amelazwa katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga
kichwani na mdomoni na mwalimu wake.
Tukio
hilo limetokea juzi majira ya saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo
alipokuwa akirejea nyumbani kwao akitokea katika malisho ya
mifugo,alipokaribia katika shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu
huyo alimkamata kijana huyo na kuanza kumcharanga kwa panga na
kusababisha kijana Limbe kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6.
“Shuhuda
wa tulio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Manoga anasema ilikuwa
kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya Limbe
iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku Limbe akiwa nyuma ya mifugo hiyo
katika barabara ambayo iko karibu na maeneo ya shule, ghafla nilimuona
mwalimu Pendo wakishikana na kijana huyo na ndipo nikamuona akiwa na
panga na kuanza kumcharanga”,alieleza.
"Nilikimbia
katika tukio na kutoa msaada kwa wote lakini, watu walijaa na kuanza
kumshambulia mwalimu Pendo kwa kumpiga ingawa jaribio hilo lilikwama
baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho Mshemas Bahai.
Mwandishi
wa habari hizi alikwenda katika kituo cha afya cha Nyashimo na kujionea
hali mbaya kwa kijana Limbe ambaye alikuwa amepoteza fahamu kwa muda wa
masaa 6 bila kujitambua na huku akiwa anaongezewa drip na kwa pembeni
mwalimu Pendo Gabriel naye akipata matibabu ya jeraha lake kichwani
ambAlo alishambuliwa na wananchi na huku akiwa chini ya ulinzi wa jeshi
la polisi.
Mwenyekiti
wa Sogesca Bahai Mshemas alisema sikukuu Krismasi imekuwa ni mbaya
katika kijiji chake baada ya wananchi wenye hasira kali kufanya
shambulio la kumshambulia mwalimu Pendo kwa kosa la kumcharanga na panga
mwanafunzi wake aliyekuwa akitokea kwenye malisho na kupita karibu na
shamba lake la mahindi akitokea katika malisho.
Hata
hivyo alisema alifanikiwa kuwatuliza wananchi wa kijiji chake na kuanza
kufanya mikakati ya kuwapeleka kituo cha afya ili wapate huduma za
matibabu.
Aliongeza kuwa walifika polisi na kuandikiwa barua ya kwenda kutibiwa wote wawili mwalimu pamoja na mwanafunzi.
Kwa
upande wake kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Dk. Ayubu
Ismail alithibitisha kuwapokea kwa majeruhi hao na kudai kuwa kijana
Limbe ndiye aliyekuwa na hali mbaya zaidi kuliko mwalimu Pendo.
Aliongeza kuwa kijana ameshonwa nyuzi 9 katika sehemu zake zote alizopatwa na majeraha na huku mwalimu akishonwa nyuzi 6.
“Ni
kweli Limbe alikuwa ametokwa na damu nyingi sana na hivyo kumpelekea
kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 lakini hali yake inaendelea vizuri
alisema Dk. Ismail”.
Na Shushu Joel- Busega
0 comments:
Post a Comment