Na. Lilian Lundo – MAELEZO - Simuyu
Idadi
ya wanafunzi wasiomudu Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) Mkoani Simiyu
imepungua kutoka wanafunzi 18,216 Machi, 2016 kufikia wanafunzi 1,614
Septemba, 2016.
Afisa Elimu wa Mkoa huo, Julius Nestory ameyasema hayo leo, Mjini Bariadi alipokuwa akifungua mafunzo kwa Maafisa wa Serikali za Mitaa wa Mkoa huo inayohusu Mawasiliano na Kushirikishana Jitihada zenye mafanikio kwenye Elimu.
“Serikali
kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-T) umeiletea
mafanikio makubwa Mkoa wa Simuyu ambapo mpaka Machi, 2016 Mkoa ulikuwa
na jumla ya wanafunzi 18,216 ambao walikuwa hawamudu KKK, idadi hiyo
imepungu na mpaka kufikia Septemba, 2016 jumla ya wanafunzi 16,602
walimudu KKK,” alifafanuna Afisa Elimu huyo.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, mafanikio hayo yamechochewa na kampeni ya Mkoa ya
kumaliza tatizo la kutokujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa wanafunzi
wa darasa la Tatu hadi la Sita ambapo walianza kwa kuwabaini wanafunzi
hao kwa majina na kuwaanzisha madarasa maalum ya KKK.
Hivyo
basi walimu waliojengewa uwezo wa mbinu za kufundisha KKK kupitia
mpango wa EQUIP-T walitumika kuwafundisha wanafunzi hao ambao waliwekwa
katika madarasa ya wasiojua KKK na kutolewa katika madarasa hayo mara baada ya kuzimudu KKK.
Vile vile Afisa Elimu huyo alisema kuwa, wanafunzi hao wamekuwa wakifundishwa muda
wa ziada wa kuanzia saa 8:30 mchana hadi saa 9:30 ambapo wazazi
waliombwa kuwasaidia chakula wanafunzi hao kwa kuwa walitakiwa kuendelea
kuwepo shuleni hata baada ya muda wa masomo ya kawaida kumalizika.
Kwa
upande wake Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Bariadi Mji, Peter Ernest
amesema kuwa Wilaya hiyo ilikuwa na jumla ya wanafunzi 1,846 wa darasa
la Tatu hadi Sita wasiomudu KKK mpaka kufikia Aprili, 2016.
Wilaya
ilianzisha madarasa rekebishi ambapo wanafunzi hao walifundishwa namna
ya kumudu KKK na kufikia Octoba, 2016 wanafunzi wote 1,846 waliweza
kumudu KKK.
Mkoa wa Simuyu ni moja ya mikoa saba iliyoko katika Mpango EQUIP-T, mikoa mingine iliyoko katika mpango huo ni Dodoma, Kigoma, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mara na Lindi.
0 comments:
Post a Comment