Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Injini
ya kuinua uchumi wa Tanzania kutoka uchumi wa chini kwenda uchumi wa
kati imetajwa kuwa ni uwepo wa umeme wa uhakika unaoendana na mahitaji.
Hayo
yamesemwa leo, mjini Dodoma na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof.
Sospeter Muhongo alipokuwa akijibu hoja mbalimabli za Wabunge zinazohusu
upataikanaji wa nishati ya umeme.
“Bajeti
ya mwaka 2016/17 itahakikisha umeme unapatikana vijijini ambapo Wizara
ya Nishati na Madini katika bajeti hii imeongezewa asilimia 50 zaidi ya
bajeti inayoisha ya mwaka 2015/2016, ili kuhakikisha umeme unapatikana
Vijijini,” alisema Mhe. Muhongo.
Mhe. Muhongo aliendelea kusema
kuwa, bajeti hiyo inahakikishha vyanzo vyote vya umeme kama vile gesi
asilia, upepo, mawimbi, makaa ya mawe, jotoardhi na jua vinazalisha
umeme Nchi nzima.
Aidha,
Waziri huyo amesema kuwa bajeti hiyo itapelekea kuboreshwa kwa
upatikanaji wa umeme kwa kupitia sheria na taratibu zinazoipa mamlaka
TANESCO peke yake kutoa huduma ya umeme kwa kuleta ushindani katika
kutoa na kusambaza umeme Nchini.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akijibu hoja kuhusu swala la kuwepo
kwa watumishi hewa na hatua zinazochukuliwa kukomesha tatizo hilo,
amesema kuwa Serikali iko tayari kufukuza Maafisa Utumishi wote ambao
wamesababisha kuwepo kwa watumishi hewa ili kubaki na Maafisa Utumishi
ambao ni wazalendo, waadilifu na wachapakazi.
0 comments:
Post a Comment