Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA
cha Mapinduzi CCM kimezidi kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi
katika uchaguzi mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Oktoba 25
baada ya kubuni mkakati mpya
wa
ushindi ambapo mgombea wa nafasi ya urais Dk. John Magufuli kuwapigia
simu wananchi akiomba wampigie kura.
Ujumbe huo unaokwenda kwa watumiaji wa simu za mitandao mbalimbali
humfikia mmiliki wa simu kupitia namba +255622333333 na mara baada ya
simu hiyo kupokelewa husikika sauti ya Dk. Magufuli akiwaomba watanzania
kumpigia kura ili aweze kushinda na hatimaye aweze kuwa rais.
Hatua hiyo ni moja ya njia muhimu za kuwafikia watanzania wote bila
kujali itikadi zao na zaidi wale baadhi ya wananchi waliokosa fursa ya
kusikia mambo yapi yatafanywa na mgombea huyo endapo kama atafanikiwa
kuwa rais.
Ukiacha utaratibu wa kampeni za moja kwa moja majukwaani, mabango,
mahojiano katika televisheni, hatua ya Chama cha Mapinduzi kubuni njia
ya kutuma ujumbe huo kwa wananchi utawasaidia kujiongezea kura katika
uchaguzi huo unaonekana kuwa na ushindani mkubwa.
Pengine hili ndio bao la mkono lililowahi kusemwa kipindi cha nyuma na
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Nape Nnauye kutokana na hatua
hiyo kuwa muhimu hususani wakati huu ambao watanzania wengi wanamiliki
simu za mkononi.
Kutokana na hatua hiyo ina maana kuwa watanzania wengi wataweza kumsikia
mgombea huyo akiwaomba kura mbali na maeneo mengine waliyozoea kusikia
sauti yake ikiomba kumchagua katika uchaguzi huo unalenga kumpata rais
wa awamu ya tano wa taifa hili.
Chama cha Mapinduzi CCM kimemsimamisha Waziri huyo wa Ujenzi kushika
kijiti kinachotarajiwa kuachwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku chache
zijazo.
0 comments:
Post a Comment