Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwigulu
Nchemba na Mgombea Ubunge Jimbo la Kisesa-Meatu Ndg.Mpina wakiwasili
Uwanja wa Mkutano hii leo wakati wa Ufunguzi wa kampeni katika Jimbo
hilo.Mapokezi ya Mgombea Ubunge Jimbo la kisesa wakati wa Mkutano wa kufungua kampeni za Ubunge na Udiwani hii leo.Mwigulu NChemba akisalimiana na Wananchi wa Kisesa hii leo alipokwenda kufanya ufunguzi wa kampeni katika Jimbo hilo.Makada wa chama cha Mapinduzi wakifuatilia Mkutano wa Kufungua Kampeni Jimbo la Kisesa.Kada
Mtiifu wa Chama cha Mapinduzi Loveness Mamuya "Iron Lady" anayeishi
Nchini Marekani ameshiriki tukio la Ufunguzi wa Kampeni wa Jimbo la
Kisesa na Zaidi amekuwa akishiriki kampeni zinazoendelea za Uchaguzi
Mkuu wa nafasi ya Madiwani.Ubunge na Urais Nchini.Loveness Mamuya
amewaomba Watanzania na Wananchi wa Kisesa kuhakikisha wanafanya
Uchaguzi wa Amani,Watu wajitokeze kupiga kura na Waichague CCM katika
nafasi zote tatu kwakua ndio chama chenye Dira na Ilani bora ya kuinua
Maendeleo ya Wananchi.,Mbali na hilo Mamuya alisisitiza kuwa atatumia
Ukada wake wa Chama cha Mapinduzi kuendelea kuwashawishi Watanzania
kuhakikisha Magufuli anashinda nafasi ya Urais kwakua rekodi ya
Uchapakazi wake inaleta matumaini kuwa Tanzania inakwenda kusonga mbele.Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Mgombea Ubunge Jimbo la Kisesa Ndg.Mpina.Mwigulu
Nchemba ambaye ameshiriki zoezi la Ufunguzi wa kampeni Jimbo la
Kisesa,Amesisitiza Watanzania kuachana na Walaghai wa kisiasa kuhusu
Mabadiliko,Amesema amabadiliko ya kimaendeleo ndio ya kuzingatia na sio
Vyama vya Siasa.Tanzania ya Mwaka 1961 na ya leo 2015 katika
elimu,Afya,Miundombinu n.k imebadilika sana,Hivyo CCM bado inanguvu ya
kuhakikisha kasi ya Kuleta maendeleo inaongezeka .Pia amesisitiza
Wananchi kujitokeza kupiga Kura kumchagua Mgombea Urais wa CCM
Ndg.J.Pombe Magufuli na Wabunge/Madiwani wote wa CCM.Sehemu ya mamia ya Wananchi wakishangilia hotuba ya Comrade Mwigulu Nchemba.Mh.Mpina
akiwa na Wazazi wake wote wawili wakati akiomba ridhaa ya kuongoza tena
jimbo la Kisesa,Kuba ameahidi kuboresha Elimu kwa kuhakikisha
anasambaza mfumo wa kutumia Computer kwenye shule zote kwasababu
alishawanunulia Sola za Umeme kwa kila Shule,Pia uboreshaji wa maji kwa
kuvuta kutoka Shinyanga kwenye mradi mkubwa unaotokea Ziwa
Victoria,Zaidi amesisitiza kuhakikisha Barabara za jimbo la Kisesa
zinafikia kiwango cha Rami.Mh.Mpina
akiwa na Kada wa Chama cha Mapinduzi kutoka DMV Marekani Bi.Loveness
Mamuya.Chama cha Mapinduzi kwa Tanzania ndio chama pekee chenye Mtandao
Mkubwa wa ndani ya Nchi na hata Nje ya Nchi,sababu inayopelekea CCM kuwa
na Wafuasi wengi kuliko chama chochote kile hapa Tanzania.
Picha na Sanga Festo Jr
0 comments:
Post a Comment