Home » » MASWI AWATOA HOFU TANESCO

MASWI AWATOA HOFU TANESCO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KATIBU Mkuu Wizara ya Nishatu na Madini, Eliakim Maswi amewatoa hofu ya kufukuzwa au kupunguzwa kwa wafanyakazi wa shirika la Tanesco kutokana na Serikali kuanzisha mkakati na mwelekeo wa kurekebisha mapungufu mbalimbali katika mfumo wa utumishi katika wizara hiyo.
Akifungua mkutano wa Kamati ya kubadilisha sekta ndogo ya umeme nchini, wenye lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za umeme, kuimarisha hali ya kifedha ya Tanesco, kuvutia wawekezaji wadogo na kupunguza ruzuku ya Serikali kwa Tanesco, Katibu huyo alisema mpango huo unalenga kumpunguzia mzigo mlaji wa umeme.
“Ili kutekeleza mpango huu ni lazima kuwe na rasilimali watu na fedha za kutosha…hatuna wazo wala mpango wa kupunguza wafanyakazi na hata kiwango cha ‘Mega watts’ zinazozalishwa," alisema Maswi. wafanyakazi.
Alisema mbali na hilo, Serikali inakuja na mpango wa kuwahakikishia usalama wa ajira, kwa kuboresha elimu zao makazini, stahili na mikataba yao, lengo likiwa kufikia tija iliyokusudiwa kupitia sekta hiyo.
Awali, Mwenyekiti Kamati ya Maendeleo Tanesco, Abdul Mkama, aliiomba Serikali kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kuondoa hofu na mashaka juu ya maslahi na ajira zao, sambamba na siasa zinazoenea mitaani kuwa shirika linavunjwa na kuundwa upya, jambo ambalo limekuwa likiwaathiri.
Serikali inakusudia kuongeza idadi ya wateja kutoka asilimia 24 hadi kufikia 50 huku pia ikikusudia kuanzisha soko huru lenye ushindani la nishati ya umeme.
Chanzo Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa