Home » » HISTORIA YA SERIKALI ZA MITAA- 3

HISTORIA YA SERIKALI ZA MITAA- 3

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Wiki iliyopita katika kona hii tulikuwa na sehemu ya pili ya historia ya Serikali za Mitaa Tanzania. Leo tunaendelea na mfululizo wa makala ile.
Tatizo la pili kubwa lililokuwa linazikabili Serikali za Mitaa ni ukosefu wa uongozi imara na watendaji wenye uwezo. Baada tu ya uhuru.
Serikali ya wananchi ilikuja na mfumo wa “Africanisation” yaani Waafrika kupewa madaraka serikalini. Kwa baadhi ilikuwa kama “Asante” kwa kushiriki katika harakati za kupigania uhuru.
Hii ilimaanisha kwamba maofisa tawala waliokuwa na uzoefu katika masuala ya Serikali za Mitaa tangu wakati wa mkoloni, walihamishiwa katika Serikali Kuu.
Dosari nyingine ilikuwa ya kuwapa wanasiasa madaraka ya watendaji. Kwa mfano, katika Halmashauri za Wilaya, wenyeviti wa Tanu walikuwa vilevile wenyeviti wa halmashauri zao na kwa halmashauri za miji na manispaa walikuwa ndiyo mameya.

Walikuwepo madiwani wa kuteuliwa
Hii ina maana kwamba wengi kati ya hao walikuwa wakithamini zaidi nafasi zao katika chama tawala. Katika hali hii baadhi yao hawakuweza kuwa viongozi imara wa kuwawakilisha vizuri wananchi katika halmashauri.
Mambo yafuatayo yalijitokeza kudhihirisha udhaifu wa madiwani wengi wa wakati huo:
Madiwani hawakuwa tayari kutekeleza kikamilifu majukumu yao, hasa kusimamia ukusanyi wa kodi, kwa kuhofia kutochaguliwa katika uchaguzi ujao.
Walijiongezea vikao ili waweze kujipatia marupurupu zaidi; wengi wao walipenda kuingilia kazi za watendaji bila ya kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa.
Wenyeviti wa halmashauri, ambao walikuwa na kofia mbili, walikuwa wakitaka wapewe marupurupu maalumu kama vile ofisi, gari, mhudumu mambo ambayo yalikuwa kinyume na utaratibu.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa