Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi amesema Serikali imejipanga kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini kufikia milioni 3.3 baada ya miaka mitatu .
Hatua hiyo inaenda sambamba na kuboresha masuala mbalimbali ikiwemo utoaji huduma ambao unalalamikiwa na watalii wengi pamoja na kuboresha ulinzi na usalama.
Akifungua Kamati ya Huduma za Watalii (TFC) hivi karibuni unaoshirikisha wadau mbalimbali wa kutoa huduma kwa watalii, alisema kwa mwaka jana ni watalii milioni 1.1 ndiyo waliingia nchini.
Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa wizara inakuja na utaratibu mpya wa kutoa mafunzo.
Akizungumzia ulinzi na usalama kwa watalii, Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Diplomasia na Watalii, Benedict Kitarike alisema matendo ya kuvamiwa kwa watalii nchini yamekuwa yakipungua kila mwaka.
Chanzo;Habari Leo
0 comments:
Post a Comment