Home » » MAGUFULI:MKANDARASI WAZAWA AJALIWE

MAGUFULI:MKANDARASI WAZAWA AJALIWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

SERIKALI imewaagiza mameneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, manispaa na majiji nchini, kutoa vipaumbele kwa makandarasi wazalendo.
Agizo hilo limetolewa wilayani hapa jana na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, wakati wa kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mji wa Manyoni.
Alisema makandarasi wazawa wamekuwa wazalendo kwa kujenga barabara bora na imara, zinazofanana na thamani ya fedha zilizotumika.
“Faida au uzuri wa makandarasi wa ndani, ni kwamba fedha wanazolipwa, zinabaki hapa hapa nchini tofauti na makandarasi wa kutoka nje ya nchi, ambao fedha tunazowalipa, wanazipeleka kwao nje ya nchi,” alisema.
Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Singida, Mhandisi Leonard Kapongo, alisema wanadaiwa zaidi ya sh. bilioni 45 na makandarasi mbalimbali.
Barabara hiyo ya urefu wa kilometa 2.4 inajengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya Gopro Construction Ltd, chini ya Mkandarasi, Prosper Shirima.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa