Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Shirika lisilo la Kiserikali la Twaweza
Hayo ni matokea ya utafiti uliofanywa Mei na Juni, mwaka jana na Shirika lisilo la Kiserikali la Twaweza na kubaini kuwa kati ya watu 20 (asilimia sita) mwenye umri wa miaka 60, ni mtu mmoja hupata fursa ya kutibiwa bure. Pia, kati ya watoto watano (asilimia 18) mtoto mmoja hutibiwa kwa mujibu wa sera.
Mtafiti wa Twaweza, Elvis Mushi, aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa ripoti ya inayotoa takwimu za huduma za sekta ya afya jijini Dar es Salaam jana.
Alisema utafiti huo ulifanyika kwa njia ya simu za kiganjani kwa uwakilishi wa kitaifa kwenye kaya 1,722 na kutembelea vituo vya afya 92.
“Takwimu hizo zilikusanywa kwa kuhusisha makundi yote yaliyohojiwa na kuitaka Serikali kutekeleza sera ya kutibiwa bure kwa watoto na wazee,” alisema.
Mushi aliongeza kuwa kutokuridhika na usimamizi wa Serikali kwenye huduma za afya, kutasababisha wananchi wasiwapeleke wagonjwa katika vituo vya afya vya Serikali.
Naye Mkuu wa Twaweza, Rakesh Rajan, alisema kuwa wazee na watoto wanaumia kwa sababu ya sera zilizowekwa na Serikali hazitekelezeki.
Alisema mara nyingi sera hizo zimekuwa ni maneno matupu,huku utekelezaji wake ukiwa mbovu kwa kushindwa kufuatilia na kutoa zawadi kwa wanaofanya vizuri ili kuongeza uwajibikaji.
“Serikali inapaswa kufuatilia utekelezaji kwa kuwachukulia hatua wahudumu wanatoa huduma duni,vinginevyo Serikali itapoteza uaminifu kwa wananchi,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment