Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
VIJANA
mkoani Simiyu wametakiwa kuacha kujiingiza katika makundi hatarishi, na
badala yake wawe wabunifu kwa lengo la kujiletea maendeleo.
Hayo
yalisemwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM)
Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga, katika sherehe ya uwekaji jiwe la msingi
katika ofisi ya wajasiriamali ya Nyasubi SACCOS mjini Bariadi.
Alisema
vijana wengi wamekuwa na dhana ya kuilalamikia Serikali kuwa
haijawaletea maendeleo, hali inayosababisha wengi wao kukaa vijiweni
ikiwa pamoja na kuingia katika vikundi vya kuhatarisha maisha yao.
Njalu
alisema kuwa maendeleo kwa kila Mtanzania yanakuja kwa kila mmoja kuwa
mbunifu pamoja na kujishughulisha katika kazi mbalimbali sambamba na
kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali.
Mwenyekiti huyo ambaye
alikuwa mgeni rasmi wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika ofisi hiyo
alisema ni vyema vijana wakawa wabunifu pamoja na kujiunga katika
vikundi mbalimbali vya wajasiriamali ili kujiletea maendeleo. Awali
akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu wa wajasiriamali wa Nyasubi
SACCOS, David Wambura, alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa asasi hiyo
jumla ya wanachama 214 wamejiunga huku wanawake wakiwa 132 na wanaume
wakiwa 82.
Alisema asasi hiyo imelenga kuwaletea maendeleo wanachama
wote kwa kujikopesha ndani ya asasi yenyewe ili kuhakikisha kuwa
wanaweza kujiletea maendeleo
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment